1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfrakano wakwamisha uchaguzi wa rais Lebanone

23 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CS9X

Muda wa mwisho kwa wabunge wa Lebanon kumchaguwa rais mpya wa nchi hiyo uko njiani kumalizika leo hii wakati mfarakano wa kisiasa ukiendelea kukwamisha uchaguzi huo licha ya shinikizo la kimataifa.

Mbunge wa muungano wa chama tawala Sollange Gemayel ameliambia shirika la habari la AFP kwamba kikao cha bunge cha juhudi za mwisho kilichopangwa kufanyika leo hii kumchaguwa mtu wa kuchukuwa nafasi ya Rais wa sasa Emile Lahoud kimeahirishwa.

Muungano huo wa chama tawala unaoipinga Syria pia hapojana usiku wa manane ulitowa wito kwa wabunge kujitokeza leo hii kumchaguwa kiongozi mpya wa taifa.

Hata hivyo mbunge mmoja wa kundi la Hizbollah linaloiunga mkono Syria ameonya dhidi ya kufanyika kwa kikao hicho.