1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Denmark kuwasilisha mswada mwishoni mwa wiki hii.

Abdu Said Mtullya10 Desemba 2009

Nchi zinazoendelea zavutana na nchi zinazoinukia kwenye mkutano wa hali ya hewa mjini Copenhagen.

https://p.dw.com/p/Kyuo
Mjumbe kutoka Bhutan kwenye mkutano wa hali ya hewa mjini Copenhagen.Picha: AP

Siku moja baada ya mkutano wa Umoja wa Mataifa unaojadili mabadiliko ya hali ya hewa kukabiliwa na mvutano mkubwa mjini Copenhagen wenyeji wa mkutano wanatazamiwa kutoa mswada rasmi wa mkataba mwishoni wiki hii.

Waziri mkuu wa Denmark Lars Lokke Rasmussen alidokeza juu ya pendekezo hilo baada ya kuhudhuria mkutano ghalfa, hapo jana.

Waziri mkuu Rasmussem alidokeza juu pendekezo hilo baada ya nchi zinazoendelea na zinazoinukia kulalamika kwamba nchi yake inaongoza mazungumzo ya mkutano kwa njia ya kuzipendelea nchi tajiri.

Lakini Wazirimkuu wa Denmark Rasmussen ameyaita malalamiko hayo kuwa ni tamthilia.Hapo awali mswada wa Denmark uliofichuka kabla ya wakati,ulipingwa na China zinazoendelea

Mfarakano mkubwa pia umetokea baina ya nchi zinazoinukia na zinazoendelea ambazo hasa ndizo zinazoathirika na madhara ya mabadiliko ya hali hewa.Kisiwa kidogo cha Tuvualu kilisababisha mfarakano huo kwenye vikao vya jana baada ya kutoa mwito wa kuanzishwa majadiliano juu kuufanyia mabadiliko mkataba wa Kyoto- yatakayoziwajibisha nchi zote kisheria.

Kisiwa hicho kidogo kilichopo kwenye bahariya Pasifik kinahofia kufunikwa na maji endapo usawa wa bahari utapanda juu zaidi .

Kwa mujibu wa pendekezo la kisiwa hicho,nchi zinazoinukia zitapaswa kuweka malengo katika kupunguza utoaji wa gesi zinazosababisha ongezeko la joto .Lakini pendekezo la kisiwa hicho linaloungwa mkono na nchi masikini ambazo hasa ndizo zinazoathirika na mabadiliko ya hali ya hewa limepingwa na China,India, Saudi Arabia na nchi zingine zinazoinukia.

Badala yake China imezinyooshea kidole nchi tajiri kwa kukataa kuchukua hatua thabiti. China imezilaumu nchi tajiri kwa kushindwa kutimiza hadi zao juu ya kupunguza gesi chafu na kutoa msaada wa fedha kwa nchi masikini ili kuziwezesha nchi hizo kupambana na madhara yanayosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

Lakini Marekani imepinga lawama hizo na imesema kwamba rais Obama ameleta mageuzi makubwa katika msimamo wa Marekani juu ya suala la mabadliko ya hali hewa.

Wajumbe kwenye mkutano wa Copenhagen wanatumai kufikia mpango hadi tarehe 18 mwezi huu juu ya kupunguza utoaji wa gesi chafu na juu ya kutenga mabilioni ya fedha kwa ajili ya kuzisaidia nchi masikini.

Mwandishi:Abdul Mtullya /AFP

Mhariri:Abdul-Rahman