1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme Bhumibol

3 Desemba 2008

Wathai na mfalme wao na siku baada yake.

https://p.dw.com/p/G8fs

Bado pande mbili zinazopingana nchini Thailand zinatumai kuwa mfalme wao Bhumibo Adulyadej atafungua mdomo na kuzungumzia juu ya hali ya machafuko katika Ufalme wake.

Kufuatia kujiuzulu kwa serikali ya Thailand,wafuasi wa Upinzani wameacha sasa kuukalia uwanja wa ndege wa Bangkok .Hatahivyo, bado watalii 230.000 wa kigeni wanasubiri kuondoka nchini kurejea makwao.

Serikali ya mpito imetangaza Desemba 8, ni siku ya kumchagua waziri mkuu mpya Bungeni. Iwapo hali ya mambo imerejea kabisa kuwa shuwari,itabidi kusubiri kuona.Bado pande zote mbili zinatumbua macho kuona mfalme wao Bhumibol (Buhmipon) anaeheshimika i kote nchini, atasema nini juu ya mgogoro huu.Yeye lakini, anaendelea kunyamaa kimya.

Mfalme Bhumibol Adulyadej (Bhumipon) wa Thailand anatambulikana kuwa mwenye kauli ya mwisho nchini hailand.Yeye yuko hata juu ya ma mlaka ya serikali.Katika maswali yote ni yeye mwenye kauli ya mwisho.Kwa muujibu wa katiba ya Thailand,yeye ndie mfalme kikatiba .Lakini kwa wathai mfalme wao ana hata mamalaka zaidi.

Thongthong Chandaransu,mtaalamu wa historia ya Ufalme wa Thailand anasema:

"Katika enzi nzima ya utawsala wake,ametumia nguvu zake zote kwa manufaa ya watu wake.Tunampenda kwasababu nae anatupenda."

Mfalme Bhumibol yuko kila wendapo nchini Thailand,kwani mabiramu yake ya hadi mita 1 yamebandikwa majumbani na hata makumbsho yake ya kale yalioshheni katika kila mji wa Thailand.Kumkosoa mfalme ni marufuku kisheria.Na hakuna yeyote anaethubutu kumbughdhi mfalme huyo hadharani.Kiasi cha miaka 2 nyuma mswisi alieishi Thailand akiwa amelewa aliichafua picha ya mfalme na akafungwa miaka 10 korokoroni.Baada ya kutumika kifungo miezi michache,mfalmed alimpa msamaha na kutolewa korokoroni.

Katika enzi ya utawala wake iliopindukia miaka 60 sasa Rama wa IX kama pia anavyoitwa mfalme huyu,thamani ya Ufalme nchini Thailand imeongezeka na hii yatokana na jinsi anavyoongoza Ufalme wake.Bhumibol daima akielewa wakati gani ni muwafaka kutia mkono wake katika siasa za nchi au lini kukaa kando.Serikali 21 zimeingia na kutoka .Mara 20 Jeshi lilinyakua madaraka na mfalme Bhumibol amebakia kitini(bukheri-mustarehe).

Hata baada ya mapinduzi ya kijeshi miaka 2 nyuma, hata majamadari walimtukuza mfalme.Kwani, bila ya ridhaa yake,serikali isingepinduka.

Tangu wapinzani hata wafuasi wa serikali ya sasa wanadai kutetea demokrasi na kuutukuza ufalme.Wathailand kutoka tabaka mbali mbali,wanaishi na kumheshimu mfalme wao ambae ijumaa hii ijayo atatimiza umri wa miaka 81.Kwa wathai ni kama Mungumtu.Na hivi mmojawao anasema:

"Ana maana kubwa kupita kiasi katika maisha yangu,kwa ukoo wangu mzima na naamini hata wathai wote wanahisi hivyo."

Hadi sasa, mfalme haingilii kati katika ugomvi wowote wa kisiasa nchini na labda kwa kuwa binafsi ni sehemu ya ugomvi wenyewe.Ubishi uliopo ni kuhusu nani atamrithi ? Baada ya kifo chake mfalme huyu mgonjwa nani atakaefuta?

Wafuasi wanaoungamkono Ufalme wanahofia kupoteza ushawishi wao.Kambi ya serikali iliotimuliwa madarakani ya wafuasi wa waziri mkuu wa zamani Thaksin,wangependa kuondoa ufalme alao hizo ni tuhuma za chama cha PAD. Yamkini hii ndio maana si Polisi, wala jeshi haikuingilia kati kuwatimua .