1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MEXICO/BELIZE:Kimbunga Dean chaelekea Mexico

21 Agosti 2007

Watu wa Mexiko na Belize wanachukua hatua za kujihami na kimbunga Dean ambacho tayari kimeshapitia Jamaica na visiwa vya Cayman.

https://p.dw.com/p/CB1u

Kimbunga hicho kilichofikia kasi ya kilometa 240 kwa saa kimeharibu nyumba na barabara, na kimeng’oa miti pamoja na kuharibu vituo vya nishati.

Watabiri wa hali ya hewa wanahofia kuwa dhoruba hiyo itakuwa kali zaidi.Hadi sasa watu wasiopungua wanane wameshakufa kutokana na kimbunga hicho kinachoelekea Mexico.

Rais Felipe Calderon wa Mexiko aliepo nchini Canada kuhudhuria mkutano amekatisha ziara yake nchini humo ili kurejea nyumbani kwa sababu ya kimbunga hicho.