1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

METTLASH : Wito juu ya Uturuki walainishwa

6 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCm6

Ujerumani na Ufaransa zimelainisha wito wao wa kutaka kuweka tarehe thabiti ya mwisho kwa Uturuki kutokana na mazungumzo yenye matatizo ya kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Nchi hizo mbili zilikuwa zikitaka kungaliwa uwezekano wa kusitishwa mazungumzo hayo kwa sababu serikali ya Uturuki inagoma kufunguwa bandari zake na viwanja vya ndege kwa Cyprus nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Katika mazungumzo ya nchi tatu huko Mettlash kati ya Ujerumani na marais wa Ufaransa na Poland Kansela Angela Merkel ameiyataka makao makuu ya Umoja wa Ulaya yalioko huko Brussels Ubelgiji kuandaa repoti ya maendeleo kufikia kipindi cha majira chipukizi hapo mwaka 2009 juu ya Uturuki kutimiza masharti ya kujiunga na umoja huo.

Kamishna anayeshughulikia kutanuka kwa Umoja wa Ulaya Olli Rehn ameelezea kufarajika kwake kwamba Merkel, Rais Jaques Chirac wa Ufaransa na Rais Lech Kaczynski wa Poland hawakudai kuwepo kwa msimamo mkali.