1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel na Sarkozy wataka ushirikiano wa karibu wa kiuchumi

Halima Nyanza(ZPR)17 Agosti 2011

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy wametoa wito wa ushirikiano wa karibu wa kiuchumi kati ya nchi zao mbili, na miongoni mwa zile zinazotumia sarafu ya Euro.

https://p.dw.com/p/12I2l
Kansela Angela Merkel na Rais Nicolas SarkozyPicha: picture alliance/dpa

Katika kujaribu kuonesha mshikamano wao  dhidi ya mgogoro wa madeni unaoikabili sasa sarafu ya Euro, viongozi hao wawili wametangaza pendekezo la kuwa na utunzaji sawa wa mahitaji ya bajeti kwa nchi hizo 17 zinazotumia sarafu ya Euro, katika katiba zao.

Nicolas Sarkozy und Angela Merkel
WakijadilianaPicha: picture alliance/dpa

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano wao mjini Paris, kansela Merkel alisisitizia kwamba nchi zote wanachama wa eneo hilo la Euro zinapaswa kufanya kazi pamoja kuimarisha udhibiti wa uchumi.

Hata hivyo wawekezaji wameonekana kukatishwa tamaa na matokeo ya mkutano huo.

Kansela Merkel na Rais Sarkozy walikuwa katika shinikizo kufikia mipango ya kuunga mkono nchi hizo za Euro na kurejesha imani ya soko baada ya msukosuko uliodumu kwa mwaka mmoja na nusu.