1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel na Sarkozy wakataa hati za dhamana za Euro

17 Agosti 2011

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy, wamependekeza hatua wanazotazamia kuwa zitasaidia kutuliza masoko ya fedha yanayoyumba.

https://p.dw.com/p/RgOF
epa02868606 German Chancellor Angela Merkel (L) and French President Nicolas Sarkozy (R) deliver a press conference at the Elysee Palace, in Paris, France, 16 August 2011. German Chancellor Angela Merkel arrived in Paris for a meeting with Sarkozy that was being closely watched by investors for signs of a more unified European approach to saving the eurozone from its mountains of debt. EPA/HORACIO VILLALOBOS +++(c) dpa - Bildfunk+++
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel(kushoto) na Rais wa Ufaransa, Nicolas SarkozyPicha: picture alliance/dpa

Wamesema, kuna haja ya kuundwa serikali ya kiuchumi katika kanda inayotumia sarafu ya Euro, kutoza kodi kwa biashara ya fedha katika nchi zote za Umoja wa Ulaya na vile vile mfumo wa kupunguza madeni ya serikali katika kanda ya Euro. Yote hayo ni mapendekezo yaliyotolewa na Merkel na Sarkozy baada ya kukutana hapo jana mjini Paris. Lengo ni kutuliza masoko ya fedha yanyoyumba barani Ulaya.

Serikali ya kiuchumi katika kanda ya Euro

Viongozi hao wamesema, lililo muhimu kabisa ni kuunda serikali ya kiuchumi ya pamoja katika nchi zinazotumia sarafu ya Euro. Tangu muda mrefu, Rais wa Ufaransa alipendekeza fikra hiyo, kwa hivyo hapo jana, alifurahi kupata fursa ya kutangaza kuwa hata Kansela wa Ujerumani, anaunga mkono pendekezo la kuunda serikali maalum ya kushughulikia sera za kiuchumi katika kanda ya Euro. Serikali hiyo ya viongozi wa nchi na serikali za nchi 17 zinazoitumia sarafu ya Euro katika Umoja wa Ulaya, itakuwa na rais atakayechaguliwa kwa kipindi cha miaka miwili na nusu. Merkel na Sarkozy wamependekeza kumpa wadhifa huo Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Herman van Rompuy.

EU-Ratspräsident Herman Van Rompuy besucht Bosnien und Herzegowina. (Oktober 2010) Copyright: Samir Huseinovic
Raisa wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Herman van RompuyPicha: DW/Samir Huseinovic

Lakini sio Sarkozy pekee aliyekubaliwa pendekezo lake. Hata Kansela wa Ujerumani amefanikiwa kuishawishi Ufaransa kuunga mkono sharti la Ujerumani la kutaka kila nchi kuwajibika kuchukua hatua imara za kupunguza madeni yake. Amesema, wanapendekeza pia kwa nchi nyingine wanachama katika kanda ya Euro, kwamba sheria ya kudhibiti madeni iwe sehemu ya katiba ya nchi. Na sheria hiyo inapaswa kuheshimiwa na kila serikali yaani hata serikali zitakazofuata. Merkel na Sarkozy wanataka pia kuanzisha kodi ya fedha zinazosafirishwa ndani ya Umoja wa Ulaya.

Dhamana za Euro sio suluhisho

Wiki ijayo, Merkel na Sarkozy wanatazamia kuyajadili mapendekezo yao pamoja na washirika wengine wa Umoja wa Ulaya. Wanachoweza kujiamulia wenyewe ni kurekebisha kodi ya mapato ya mashirika katika nchi hizo mbili. Lakini Merkel amesema, makampuni ya Kijerumani hayatotozwa kodi zaidi. Na pendekezo la utata la kuanzisha hisa za euro zitakazodhaminiwa na nchi za kanda ya Euro, limepingwa na Merkel na Sarkozy. Wanasema hilo si suluhisho.

Merkel amesema, mara kwa mara, husikia kuwa dhamana za Euro ndilo suluhisho. Kwa maoni yake, Ulaya haijafikia umbali wa kuhitaji ufumbuzi huo. Vile vile yeye wala haamini kuwa hisa za euro zitatenzua matatizo ya deni katika kanda ya Euro. Anaamini kwa kufuata utataribu sahihi, imani ndio itakapoweza kurejea katika masoko ya fedha hatua kwa hatua. Jawabu sio dhamana za Euro.

Mwandishi: Junghans,Daniela/ZPR

Mhariri:Josephat Charo