1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel na Sarkozy kumshawishi Medvedev kuhusu NATO

Admin.WagnerD19 Oktoba 2010

Kansela Angela Merkel na Rais wa Ufaransa Nikolas Sarkuzy wanakutana na Rais wa Urusi Dmitry Medvedev leo (19 Oktoba 2010) nchini wa Ufaransa kumshawishi Medvedev aikurubishe zaidi nchi yake na Ulaya

https://p.dw.com/p/PhTg
Kutoka kulia: Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy na Rais wa Urusi Dmitry Medvedev katika hoteli ya Royal mjini Deauville, Ufaransa, 19 Oktoba, 2010. (AP Photo/Remy de la Mauviniere/Pool)
Kutoka kulia: Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy na Rais wa Urusi Dmitry Medvedev katika hoteli ya Royal mjini Deauville, Ufaransa, 19 Oktoba, 2010. (AP Photo/Remy de la Mauviniere/Pool)Picha: AP

Kutokea madirisha ya hoteli ya Royal, Angela Merkel na Nicolas Sarkuzy wanaangazia mkondo wa mambo. Muangaza wao wa mwanzo ulikuwa ni wa jana Luxemburg, ambako mawaziri wa fedha wa Ulaya walikutana. Mkutano huu ulikuwa unaangalia kwa namna gani Ulaya inaweza kupambana na mgogoro wa kifedha katika siku za usoni.

Msimamo wa Pamoja wa Kifedha

Bila ya shaka, yale yanayotokea Ugiriki yanatoa funzo la pekee kwa Paris na Berlin kwamba lazima zifanye jitihada za kutosha kuhakikisha kwamba hayasambai katika nchi zao, kama anavyosema Sarkuzy: "Mgogoro wa kifedha umeonesha namna gani ni muhimu kufanya mageuzi kwenye mchakato wetu wa kifedha, kurekebisha nakisi na kuuendesha vyema mfumo wetu wa kisiasa na kiuchumi. Kwa hivyo tutapeleka pendekezo moja la Ufaransa na Ujerumani kule Brussels: Serikali ambayo baada ya miezi sita itakuwa haijapiga hatua kubwa dhidi ya nakisi, italazamika kulipia"

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel (kushoto) akiwa na Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy katika mkutano na waandishi wa habari hapo jana (18 Oktoba 2010), mjini Deauville, Ufaransa. (AP Photo/Franck Fife, Pool)
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel (kushoto) akiwa na Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy katika mkutano na waandishi wa habari hapo jana (18 Oktoba 2010), mjini Deauville, Ufaransa. (AP Photo/Franck Fife, Pool)Picha: AP

Pendekezo hili la serikali mbili linakusudia kusema kwamba moja kwa moja Wafaransa watawawekea vikwazo wale ambao hawakutimiza sharti la kupunguza nakisi za uchumi wao, na jambo hili limefurahiwa na Kansela Merkel. Ingawa pia, litamaanisha kubadilishwa kwa baadhi ya vipengele vya makubaliano ya Umoja wa Ulaya katika masuala ya fedha na uchumi.

"Tunahitajika kufanya maerekebisho ya mkataba, hasa vile vipengele ambavyo vnahusiana na masuala kama haya ya mgogoro wa kifedha, ili tuweze kujenga imani na uwezo wa kupambana na matatizo kama haya. Ni muhimu hasa kutafuta chombo ambacho kitakuwa na jukumu la yote haya. Na hilo ndilo somo tulilojifunza kutokana na mgogoro huu wa kifedha." Anasema Kansela Merkel.

Msimamo Mmoja Kuhusu NATO na Urusi?

Wakati katika suala la kiuchumi, nchi hizi mbili zimetoka na msimamo wa pamoja, suala ni ikiwa pia zitakuwa na msimamo mmoja katika mpango wa makombora ya kujilinda ya ya Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi, NATO. Na hili ndilo linaloangaliwa katika mkutano wao wa leo (19 Oktoba 2010) wa pande tatu, ambapo Sarkuzy na Merkel wanakutana na Rais Dmitry Medvedev wa Urusi.

Kwa siku za karibuni, Urusi imekuwa ikiutilia mashaka sana mpango huo wa NATO, lakini Merkel na Sarkuzy wanataka Urusi ifanye kazi karibu sana na NATO, hasa kwa kuwa zama za vita baridi zimepita. Bila ya shaka, jambo hili litaifanya pia Urusi kupunguza sio tu wasiwasi wake, bali pia udhibiti wake katika nchi zilizokuwa Kambi ya Mashariki katika siku za vita baridi, kitu ambacho ni kigumu kwa taifa hilo.

Mwandishi: Mohammed Khelef/Johannes Durchrow/ZPR

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman