1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel na Bush kutafuta suluhisho la kidiplomasia

P.Martin12 Novemba 2007

Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel amekamilisha majadiliano yake pamoja na Rais wa Marekani, George W.Bush yaliyofanywa nyumbani kwa Bush kwenye shamba lake mjini Crawford, Texas.

https://p.dw.com/p/CB0j
Kansela Merkel na Rais Bush baada ya kuzungumza na waandishi wa habari uliofanywa kwenye shamba lake katika mji wa Crawford,Texas
Kansela Merkel na Rais Bush baada ya kuzungumza na waandishi wa habari uliofanywa kwenye shamba lake katika mji wa Crawford,TexasPicha: AP

Katika mkutano wao pamoja na waandishi wa habari,Merkel na Bush waliahidi kuendelea kutafuta suluhisho la kidplomasia kuhusu mgogoro wa mradi wa nyuklia wa Iran.

Merkel akasema,ataunga mkono duru nyingine ya vikwazo dhidi ya Iran ikiwa Iran itaendelea kupinga mwito wa jumuiya ya kimataifa kusitisha harakati za kurutubisha madini ya uranium.

Kansela Merkel akaongezea kuwa walijadiliana pia kwa kirefu,mkutano wa hali ya hewa utakaofanywa Bali nchini Indonesia na anaamini mkutano huo una nafasi nzuri ya kufanikiwa.