1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel atetea uamuzi wa benki ya Ulaya, ECB

8 Septemba 2012

Kansela Angela Merkel ameitetea benki kuu ya Ulaya Ijumaa (07.09.2012) baada ya mpango wake wa kununua madeni ya mataifa ya eneo la euro kuzusha malalamiko nchini Ujerumani .Nakitisho cha kuzuwia mpango huo.

https://p.dw.com/p/165Kd
Austrian Chancellor Werner Faymann (R) and German Chancellor Angela Merkel brief the media during a news conference in the Chancellor's office in Vienna September 7, 2012. Merkel is on a one-day visit to Austria. REUTERS/Herwig Prammer (AUSTRIA - Tags: POLITICS)
Kansela Angela Merkel akiwa mjini ViennaPicha: Reuters

Rais wa benki kuu ya Ulaya, ECB Mario Draghi amewasilisha mipango siku ya Alhamis ya kununua dhamana kwa kiasi kisicho na ukomo zinazopevuka katika muda wa miaka mitatu zilizotolewa na mataifa ambayo yameomba fedha za uokozi kutoka mfuko wa uokozi wa Ulaya na kutimiza masharti magumu ya sera za ndani. Mkuu wa benki kuu ya Ujerumani alikuwa pekee aliyepinga mpango huo wakati wa kufikiwa uamuzi huo.

Hessen/ Der Praesident der Europaeischen Zentralbank (EZB), Mario Draghi, fasst sich am Donnerstag (06.09.12) in Frankfurt am Main auf einer Pressekonferenz zu den Ergebnissen der Ratssitzung ans Kinn. Die Europaeische Zentralbank (EZB) hat den unbegrenzten Kauf von Anleihen der Euro-Krisenstaaten beschlossen. Das erklaerte EZB-Praesident Mario Draghi am Donnerstag nach der Sitzung des Notenbankrats in Frankfurt am Main. (zu dapd-Text)
Rais wa benki kuu ya Ulaya ECB ,Mario DraghiPicha: dapd

Vyama vinavyounda serikali ya mseto vya nadharia za mrengo wa kati-kulia vinaendelea kwa kiasi kikubwa kuwa nyuma ya msimamo wa Merkel wa kuunga mkono wa kuyapa msaada mataifa yaliyo katika matatizo kama Uhispania na Italia lakini kwa masharti kuwa yanatekeleza mageuzi magumu ya kifedha katika nchi zao.

Kuna malalamiko

Lakini malalamiko kutoka kwa kundi dogo lakini lenye sauti linalotia shaka shaka kuhusu mradi wa Ulaya miongoni mwa wabunge wa chama cha Kansela Merkel pamoja na vyombo muhimu vya habari vya kihafidhina yanaonyesha hofu ya kisiasa katika kipindi kinachoelekea kwenye uchaguzi ambao utafanyika mwaka mmoja kutoka hivi sasa.

ECB ni taasisi huru na yenye nguvu kubwa , Merkel amewaambia waandishi habari mjini Vienna, akisisitiza kuwa msaada utatolewa ukiambatana na masharti, hayo yakiwa ni matamshi yake ya kwanza kuhusiana na mpango huo.

''Masharti ni suala muhimu sana. Udhibiti na msaada, ama udhibiti na masharti, vinakwenda sambamba''. amesema Merkel.

Wajerumani wana wasi wasi

Lakini Wajerumani wengi wahafidhina wanakubaliana na wasi wasi wa Jens Weidmann , mkuu wa benki ya Ujerumani, Bundesbank, kuwa mpango wa ununuzi wa dhamana unakwenda kinyume na suala nyeti la kuyapa fedha mataifa yenye nakisi katika bajeti zao, kuondoa mbinyo kutoka katika serikali wa kufanya mageuzi na hatimaye utaongeza ughali wa maisha.

Bundesbankpräsident Jens Weidmann sitzt am Dienstag (13.03.2012) in Frankfurt am Main bei der Jahrespressekonferenz der Bundesbank. Die Staatsschuldenkrise im Euroraum hat tiefe Spuren in der Bilanz der Deutschen Bundesbank hinterlassen. Der Gewinn der Notenbank schrumpfte auf 643 Millionen Euro. «Der Grund für den Rückgang des Gewinns findet sich vor allem in der Erhöhung der Risikovorsorge», erklärte Bundesbankpräsident Jens Weidmann am Dienstag in Frankfurt. Foto: Boris Roessler dpa/lhe
Mkuu wa benki kuu ya Ujerumani Bundesbank, Jens WeidmannPicha: picture-alliance/dpa

Kuyapatia fedha za bure mataifa yenye madeni, ilikuwa kichwa cha habari katika gazeti lenye wasomaji wengi la Bild, ikiwa ni ukosoaji mkali kwa mikopo iliyopatiwa Ugiriki pamoja na mataifa mengine ya eneo la euro ambayo yamo katika matatizo, na kuongeza kuwa hatua ya ECB inaweza kuiporomosha sarafu ya euro.

Uchunguzi wa maoni

Uchunguzi wa maoni uliotolewa Alhamis, (06.09.2012) kabla ya mpango wa ununuzi wa dhamana kutangazwa unaonesha karibu Mjerumani mmoja kati ya wawili hawana imani na Draghi, ambaye ni Mtaliani.

Sachsen/ Der CDU-Bundestagstagsabgeordnete Klaus-Peter Willsch fuehrt am Montag (14.11.11) in Leipzig bei seiner Rede auf dem 24. Bundesparteitag der CDU seine Argumente gegen den Europaeischen Rettungsschirm aus. Der kuenftige Europa-Kurs der CDU, das Thema Mindestloehne und neue Wege in der Bildungspolitik stehen im Mittelpunkt des 24. Bundesparteitags der Christdemokraten. (zu dapd-Text) Foto: Sebastian Willnow/dapd
Mbunge wa chama cha CDU Klaus-Peter WillschPicha: dapd

Wabunge kadha wameapa kuchukua hatua ya kisheria kuzuwia mpango huo. ''Tunapaswa kufikiria kuchukua hatua za kisheria kuangalia iwapo ECB imekiuka kwa kiasi kikubwa mamlaka yake. Nina hakika kuwa hii ndio hali halisi''. Amesema Klaus-Peter Willsch, mbunge ambaye hana imani na mradi wa Ulaya moja kutoka chama cha kansela Angela Merkel cha Christian Democratic Union, CDU, katika mazungumzo na radio ya Ujerumani.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre/afpe

Mhariri: Daniel Gakuba.