1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel akutana na Sarkozy karibu na Paris

Hamidou, Oumilkher11 Oktoba 2008

Viongozi wa Ufaransa na Ujerumani wakutana kabla ya mkutano wa kilele wa umoja wa ulaya kesho katika mji mkuu huo wa Ufaransa

https://p.dw.com/p/FY7B

Paris:


Kansela Angela  Merkel wa Ujerumani na rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy wameahidi kushirikiana kwa dhati katika kukabiliana na mzozo kataika masoko ya fedha ulimwenguni.Kuna masoko yaliyopindukia yanayobidi kuingizwa katika mfumo wa kijamii,amesema hayo kansela Angela Merkel weakati wa mkutano pamoja na rais Sarkozy katika eneo la mashariki la Colombey-les Deux-Eglises.Rais Nicolas Sarkozy amesisitiza  juu ya umuhimu wa kuendelezwa hali ya kuaminiana na ushirikiano wa dhati kati ya Ufaransa na Ujerumani kwa Umoja wa ulaya.Viongozi hao wawili wamezindua kumbusho la rais wa zamani wa Ufaransa Charles de Gaule huko Colombey.Kesho viongozi wa Umoja wa ulaya watakutana mjini Paris kuzungumzia mzozo katika maswoko ya fedha ulimwenguni.