1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MDC chasema Zanu Pf kinapanga vurugu Zimbabwe

6 Aprili 2008

-

https://p.dw.com/p/Dco4

HARARE

Kiongozi wa Upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai ameonya kwamba chama tawala Zanu PF huenda kikatumia duru ya pili ya uchaguzi wa rais kumrudisha madarakani rais Robert Mugabe kwa kutumia nguvu.Tsvangirai amepinga duru ya pili ya Uchaguzi akidai kwamba amepata ushindi wa wazi katika uchaguzi war ais uliofanyika mwishoni mwa juma lililopita.

Amedai chama tawala kiko kwenye harakati za kuwakusanya watu watakaoanzisha ghasia na fujo nchini humo.

Madai hayo yamekanushwa na chama tawala ambacho kimesema MDC kinajaribu kuanzisha hali ya wasiwasi nchini humo.

Matokeo ya uchaguzi wa rais hayajatangazwa lakini chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change MDC kimesema leo kitaanzisha tena jaribio katika mahakama kuu ya Zimbabwe ya kutaka matokeo ya uchaguzi huo yatangazwe mara moja.Hata hivyo taarifa za hivi punde zinasema chama tawala kimeitaka tume ya uchaguzi kuhesabu upya kura za uchaguzi wa rais kwasababu kumekuwa na makosa kadhaa katika shughuli ya kuhesabu kura hizo.Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ameitaka tume ya uchaguzi kutangaza haraka matokeo ya uchaguzi wa rais ili kuepusha ghasia nchini humo huku rais Thabo Mbeki akitoa mwito wa kuwepo subira kwa upande wa upinzani.Mapema hapo jana polisi waliokuwa na silaha waliwazuia mawakili wa chama cha MDC kuingia kwenye mahakama hiyo.Wakati huohuo tume ya uchaguzi imetangaza matokeo yote ya uchaguzi wa viti vya bunge la seneta matokeo hayo yanaonyesha chama cha rais Mugabe kimepata viti 30 katika bunge la juu sawa na chama cha upinzani huku upinzani ukinyakuwa viti 109 katika bunge dogo na Zanu PF kikapata viti 97 hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa chama hicho kushindwa kupata wingi wa viti bungeni tangu nchi hiyo ijipatie uhuru kutoka kwa waingereza mwaka 1980.