1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi waufuta mchuano wa kirafiki wa Ujerumani

18 Novemba 2015

Mchuano wa kirafiki wa kimataifa kati ya Ujerumani na Uholanzi uliotarajiwa kuchezwa Jumanne usiku ulifutwa kutokana na hofu ya mashambulio ya ugaidi. Kansela Merkel ni miongoni mwa waliotarajiwa kuhudhuria

https://p.dw.com/p/1H7kD
Stadion Hannover HDI Arena Deutschland Niederlande
Picha: Getty Images/A.Koerner

Mchezo huo uliopangwa kuchezwa katika uwanja wa HDI Arena, WA klabu ya Hannover, ulifutwa dakika 90 kabla ya kuanza, baada ya kutokea taarifa kuwa kulikua na mpango wa kufanyika mashambulizi ya kigaidi ndani ya uwanja.

Watu waliokuwa tayari wamefika uwanjani humo walilazimika kuondolewa nje ili polisi wafanye uchunguzi kuhusiana na kitisho hicho cha shambulizi. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alikua miongoni mwa watu waliotarajiwa kuhudhuria mchezo huo katika uwanja huo wenye uwezo wa kuwa na watazamaji 49,000.

Aidha mpambano mwingine uliofutwa jana kwa hofu ya ugaidi ni kati ya Ubelgiji na Uhispania uliokua ufanyike nchini Ubelgiji.

Kwingineko, kule Uingereza, mashabiki waliofurika uwanjani walionyesha mshikamano na taifa la Ufaransa wakati wa mchuano wa kirafiki katika wenyeji Uingereza na Ufaransa. Kila mtu aliyefika uwanjani Wembley aliimba wimbo wa taifa wa Ufaransa kabla ya kuanza dimba hilo ili kuwakumbuka wahanga wa mashambulizi ya Paris. Uingereza iliibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Abdulrahman