Mazungumzo ya Bali yaongezwa muda kwa siku moja | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 15.12.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Mazungumzo ya Bali yaongezwa muda kwa siku moja

BALI

Mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa mjini Bali nchini Indonesia umneongezwa muda kwa siku moja zaidi wakati wajumbe wakiwa ukingoni kufikia muafaka wa makubaliano.

Ulaya na Marekani hadi sasa zimeshindwa kukubaliana juu ya viwango vya kupunguza utowaji wa gesi zenye kuathiri mazingira duniani.

Umoja wa Ulaya unataka mataifa ya kitajiri yenye maendeleo makubwa ya viwanda kupunguza utowaji wa gesi hizo kwa hadi asilimia 40 ifikapo mwaka 2020 lengo ambalo serikali ya Marekani inalipinga.

Stavros Dimas mkuu wa masuala ya mazingira wa Umoja wa Ulaya anasema wanaendelea kusisitiza kujumuisha kutajwa kwa dokezo la viwango utowaji wa gesi chafu zinazoathiri mazingira kwa nchi zilizoendelea ifikapo mwaka 2020 ambavyo vitazingatia ushauri wa jopo la wanasayansi la IPCC na kusisitiza kwa mara nyegine tena kwamba mpango wa Bali wa kukabiliana na ongezeko la ujoto duniani lazima ujuwe mahala unakoelekea.

Mazungumzo hayo ya Bali yanakusudia kuweka miongozo kwa ajili ya kuanza mazungumzo rasmi ya miaka miwili juu ya mkataba wa kuchukuwa nafasi ya Itifaki ya Kyoto ambayo muda wake unamalizika hapo mwaka 2012.

 • Tarehe 15.12.2007
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/Cbxq
 • Tarehe 15.12.2007
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/Cbxq

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com