1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazishi ya kitaifa ya marehemu Rais Lansaba Conte wa Guinea kufanyika leo

Mohamed Dahman26 Desemba 2008

Kiongozi wa mapinduzi wa Guinea Kepteni Moussa Didis Camara amesema kwamba marehemu Rais Lansana Conte atazikwa kwa heshima ya taifa baadae leo hii.

https://p.dw.com/p/GNL1
Marehemu Rais Lansana Conte wa Guinea.Picha: picture-alliance/dpa

Conte amefariki hapo Jumaatatu baada ya kuitawala nchi hiyo ya Afrika Magharibi kwa miaka 24.Masaa machache baadae kundi la kijeshi la Camara lilidhibiti vyombo vya habari vya nchi hiyo na kutangaza mapinduzi.Camara baadae ameahidi kwamba ataitisha uchaguzi baada ya miaka miwili.

Camara amesema baraza lake la taifa litaitisha uchaguzi huru,wa kuaminika na wa wazi ifikapo mwezi wa Desemba mwaka 2010.

Hapo jana Waziri Mkuu Ahmed Tidiane Souare ambaye awali alipinga mapinduzi hayo ameahidi kumuunga mkono Camara.Umoja wa Mataifa,Umoja wa Afrika,Umoja wa Ulaya na Marekani zote zimelaani mapinduzi haya ya kijeshi na kutowa wito wa kukabidhiana madaraka kwa njia ya kidemokrasia.

Viongozi hao wa kijeshi wamewaalika wanadiplomasia wa kigeni katika mkutano hapo kesho mjini Conakry kuwahakikishia jumuiya ya kimataifa dhamira yao.