1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mauaji ya 'halaiki' yameanza tena Sudan Kusini

Jane Nyingi
13 Aprili 2017

Upo wasiwasi mkubwa kuwa mapigano yanayoendelea kwa sasa nchini Sudan Kusini ni mauji ya Kimbari  ambayo yanafanywa kwa misingi ya kikabila amesema waziri wa maendeleo ya kimataifa wa Uingereza Priti Patel.

https://p.dw.com/p/2bBO7
Südsudan Kämpfer
Picha: picture alliance/AP Photo/J. Lynch

Waziri Patel  amewataka viongozi kutoka mataifa ya kigeni  kufanya juhudi zaidi kuishinikiza serikali ya Sudan Kusini kuumaliza mgogoro  ambao umesababisha vifo vya maelfu ya watu. Akizungumza na waandishi wa habari punde baada ya kukamilisha ziara yake katika taifa hilo changa zaidi duniani, waziri huyo wa Uingereza  alisema alichokiona ni cha kusikitisha, kuanzia msako wa nyumba hadi nyumba kuwatafuta na kisha kuwaua wapinzani wa serikali hadi kuteketezwa vijiji wanamoishi.  Akinamama katika vijiji hivyo pia wamebakwa huku  serikali ya rais Salva Kiir ikitumia chakula kama silaha  ya vita, kwa kuzuia chakula cha msaada kufika maeneo ya upinzani. Waziri huyo pia alitembelea kambi kadhaa nchini Uganda zilizowapa hifadhi zaidi ya wakimbizi  lakini nane wa Sudan Kusini. Maelfu ya wakimbizi wanaendelea  kuvuka mpaka  kufuatia ripoti za mauji ya kikabila.

Manuela - Flucht aus dem Südsudan in die Dürre
Wasudan Kusini wanaotoroka vitaPicha: DW/S. Petersmann

Wakimbizi hao wanasema mashambulizi ya sasa yanafanywa na vikosi vya serikali kutoka kabila la rais Salva Kiir la Dinka na yawalenga watu wa kabila la aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar la Nuer. Watu kutoka makabila mengine madogo wanaoshukukiwa kuwaunga mkono wapinzani wa serikali, pia wamekuwa wakilengwa katika mashambulizi hayo. Password Okot ni mmoja wa wakimbizi hao,“Nilikuwa na ndugu wawili; mmoja wao alikamatwa na askari na kuchinjwa bila sababu. na mwingine alikuwa akijaribu kutoroka lakini akapigwa risasi. Mimi   sijui nifanye nini na wake zao na watoto.Bado  niko katika hali ya mshtuko na huzuni nyingi hivi sasa.Nimefikiria hata  kurejea tena katika kijiji changu ili mimi pia niuliwe .Ni uchungu usioweza kustahimilika.”

Viongozi wa Afrika wasalia kimya

Wakati wa ziara yake nchini Sudan Kusini waziri wa Uingereza pia alikutana na rais Salva Kiir. Patel amewakosoa viongozi wa Afrika kwa kutoishinikiza serikali ya Sudan Kusini kusitisha mauji na machaufuko, badala ya kusubiri ufumbuzi kutoka mataifa ya bara jingine.

Außenminister Gabriel zu Besuch im Kosovo
Waziri wa maswala ya kigeni Ujerumani Sigmar GabrielPicha: picture alliance/dpa/M.Skolim

Ujerumani ni miongoni mwa mataifa yaliyotoa usaidizi wake Sudan Kusini hasa kwa wanaokabiliwa na njaa kama asemavyo waziri wa maswala ya kigeni Ujerumani Sigmar Gabriel.“Sisi tunafanya hivi kutokana na mahitaji ya msaada wa kiutu,na pia kwasababu tunaamini ni swala la heshima kuwa bara ulaya, kuwa mjerumani  na pia jukumu letu la kuwajibika katika jamii ya kimataifa  kwa kutoa usaidizi ili kuhakikisha angalau watu wanasalimika.”Shirika la Umoja wa mataifa linakadiria  watu wapatao millioni tatu wametoroka makwao kutokana na vita hivyo huku wengi wao wakipata hifadhi katika taifa jirani la Uganda. 

Mwandishi;Jane Nyingi/AFP/APE
Mhariri:Yusuf Saumu