1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mauaji mapya yazusha wasiwasi nchini Kenya

27 Januari 2008

Si chini ya watu 10 wameuawa hii leo katika mapambano yaliyozuka katika Bonde la Ufa nchini Kenya huku Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan akijaribu kutenzua mgogoro wa mwezi mmoja nchini humo.

https://p.dw.com/p/CyPr
Residents are protected by the police as they flee during ethnic clashes, Sunday, Jan. 27, 2008 in Naivasha some 100 kilometers from Nairobi, Kenya. Gangs armed with machetes and bows and arrows burned and hacked to death members of a rival tribe in western Kenya Sunday, as the death toll from the latest explosion of violence over disputed presidential elections rose to at least 69. Houses were blazing in the center of Naivasha, a tourist gateway. (AP Photo/Karel Prinsloo)
Wakaazi wanaokimbia mapigano Naivasha walindwa na polisiPicha: AP

Ripoti kutoka Naivasha zinasema watu 6 wamechomwa moto na 4 wengine wameuawa kwa kupigwa mapanga.Sasa si chini ya watu 60 wameuawa katika machafuko ya siku mbili zilizopita magharibi mwa Kenya.

Siku ya Jumamosi,baada ya kutembelea maeneo yaliyokumbwa na machafuko katika Bonde la Ufa,Annan alionya kuwa ghasia zilizozuka kufuatia kuchaguliwa tena kwa Rais Mwai Kibaki Desemba mwaka jana,sasa si mgogoro unaohusika na uchaguzi bali ni tatizo kubwa la ukiukaji wa haki za binadamu.Kiongozi wa upinzani Raila Odinga anamtuhumu Kibaki kuwa uchaguzi wa Desemba ulifanyiwa udanganyifu.

Hii leo,Kofi Annan baada ya kukutana na Odinga alitoa mwito kwa pande mbili zinazohasimiana kuwateua maafisa wanne kufanya majadiliano zaidi.Hali ya wasiwasi imezuka,kwa sababu ya mapambano yaliyotokea katika miji ya Naivasha na Nakuru.Takriban watu 800 wameuawa na kama watu laki mbili na nusu wamekimbia makaazi yao tangu kuzuka kwa machafuko yanayohusika na matokeo ya uchaguzi wa rais.