1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matokeo ya uchaguzi wa Zimbabwe yachelewa

1 Aprili 2008

Matokeo ya uchaguzi wa zimbabwe yanatirrika pole pole na kuna shaka ya kupitishwa mizengwe.

https://p.dw.com/p/DYo7

Kutangazwa matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa Zimbabwe kunaendelea kucheleweshwa.Bado pia si wazi iwapo rais asiependeza machoni mwa wengi -Robert Mugabe atabakia madarakani kwa kipindi kingine cha miaka 6 cha utawala au chama cha upinzani cha MDC chini ya Morgan Tsvangirai kitashika madaraka.Uchambuzi wa Johannes Beck:

►◄

Kwa mwendo wa konokono, matokeo ya uchaguzi wa zimbabwe wa jumamosi yanatoka mjini Harare,mji mkuu wa zimbabwe .Tume ya uchaguzi ya Zimbabwe -ZEC- inahesabu bila vishindo kura tena kwa aina ambayo yamfanya mtu kutia shaka jungu linapikwa nyuma ya pazia kufanya mizengwe ili kumtawaza kitini rais M;ugabe kwa awamu nyengine.

Chama cha upinzani cha MDC ,kwa makisio yake ya kura kilivyohesabu,kinaongoza wazi.Hata chama-tawala cha ZANUpf kinahisi vivyo hivyo.

Uchunguzi huru nani hasa anashinda kwa sasa ni vigumu.Hatahivyo, kwamba rais Mugabe ameweza kuwasadikisha wazimbabwe wamchague tena kwa sura ya hali ya mambo ilivyo chini ni miujiza.Kwani,sio yeye alieifilisi nchi hii na kuufikisha ughali wa maisha hadi laki 100.Hilo si debe zuri kupiga ili kujitembeza.

Hata kabla ya uchaguzi, chama kinachotetea haki za binadamu cha Amnesty International na kile cha Human Rights Watch vimelalamika juu ya kamatakamata ovyo kwsa wapinzani, vyombo vya habari vya dola kuripoti upande mmoja tu ule wa serikali na kununua kura.

Hiyop haikutoa nafasi ya kampeni huru na ya haki ya uchaguzi huu.

Isitoshe, wachunguzi wa uchaguzi wa kimataifa waliteuliwa kutoka zile dola rafiki kama vile China,Urusi au Iran,na kuwa nchi jirani za kiafrika -SADC zimeshiriki ni jambo linalo kera.

Inakera pia kuwa hata kutoka nchi jirani inayotawaliwa kidemokrasi ya Msumbiji,hakuna sauti iliopazwa kunungunika yaliopita Zimbabwe.Rais wa zamani wa Msumbiji Joaquim Chissano akizungumza na Deutsche Welle alidai eti hana haki ya kutilia shaka nia njema ya kiongozi mwenzake.Na kiongozi mwenyewe wa Zimbabwe anadai uchaguzi huu umepita bila maonevu,ulikua huru na wazi kabisa.

Tabia hii alionesha rais wa zamaniw a Msumbiji Chissano ni tabia hasa wanayoonesha viongozi wa kiafrika zinapokanyagwa kwa mguu haki za binadamu na uongozi mbaya wa utawala katika nchi jirani .Tabia yao ni kufumba macho na mdomo.Huo ndio mshikamano muovu unaooneshwa na viongozi wa kiafrika.

Yule anaetaka kukua na kuendelea mbele,anabidi pia kuridhia kukosolewa na kuvumilia .Kuna mifano michache kama vile mfumo wa African Peer Review Mechanism -mfumo ambao nchi zakosoana uongozi wa serikali zao.

Ulimwengu wa nje wasemaje ?

ikiwa kama ilivyotarajiwa serikali za Umoja wa Ulaya zimeueleza ucahguzi wa Zimbabwe si wa haki wala na huru,ni msimamo barabra.Zinapaswa kuendelea kuishinikiza Zimbabwe na kudai demokrasia zaidi.

Lakini nchi za Ulaya nazo pia zifunue mdomo na kutoa mfano mwema inapokanyagwa haki za binadamu na uhuru wa maoni hata pasipohusika na masilahi ya ardhi za wakulima wa kizungu .Kwani sio Zimbabwe tu ambako haki za binadamu zinapondwa -ziseme ikiwa ni Libya,Gambia au Ethiopia.