Matokeo ya michezo mwishoni mwa Juma | Michezo | DW | 30.10.2006
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Matokeo ya michezo mwishoni mwa Juma

Bremen bado inashika usukani katika Bundesliga, i Manchester United inaongoza ligi ya England na Jee Al Ahli itaweza kutamba mbele ya Sfaxien ya Tunisia mjini Tunis ?

Mchezaji wa Stuttgart Mbrazil Cacau (kulia) akiwania mpira wa juu na Dario Rodriguez kutoka Uruguay anayechezea Schalke 04, wakati wa pambano lao Jumapili. Stuttgart ilishinda 3-0 .

Mchezaji wa Stuttgart Mbrazil Cacau (kulia) akiwania mpira wa juu na Dario Rodriguez kutoka Uruguay anayechezea Schalke 04, wakati wa pambano lao Jumapili. Stuttgart ilishinda 3-0 .

Kilabu ya Werder Bremen bado inashikiliausukani wa ligi hiyo baada ya kuitandika vibaya FSVMainz 05 mabao 6-1 na mechi yaJumapili kati ya Schalke na Stuttgart kumalizika kwa Schalke kurudi nyumbani mjini Gelsenkirchen na pigo la mabao matatu kwa bila. Matokeo hayo yamebadili msimamo wa ligi hiyo, kwa Bayern Munich kujisogeza nafasi ya pili katika kinyanganyiro hicho baada ya kushinda nyumbani wa mabao 2-0 dhidi ya Eintracht Frankfurt.

Wakati Bremen ina pointi 19, Bayern ina pointi 16 sawa na Schalke lakini ikiitangulia kwa wingi wa magoli. Katika baadhi ya mechi nyengine za Bundesliga, Bayer Leverkusen iliibwaga Borussia Monchen Gladbach nyumbani kwao mabao 2-0, Cottbus ikatamba nyumbani mbele ya wageni wao Hertha Berlin, Hamburg ikatoka sare nyumbani na Hannover 96 bila ya kufungana,Nurenberg ikatoka pia sare ya bao moja kwa moja na Borussia Dortmund.

Habari kutoka Uingereza zinasema kilabu mbili Celtic ya mjini Glasgow Scotland na Tottenham ilioko katikaligi kuu ya England- Premier League, huenda zikawana nia ya kutaka kumsajili aliyekua mchezaji na nohodha ya zamani wa timu ya taifa ya England David Beckham kutoka real Madrid ya Uhispania.Beckham mwenye umri wa miaka 31 amekua si mchezaji wa kutegemewa katika kikosi cha kawaida cha Real msimuhuu na mkataba wake na miamba hiyo ya Uhispania utamalizika mwaka ujao 2007.

Meneja wa Celtic Gordon Strachan alinukuliwa na gazeti la Sunday telegraph akisema hapo jana kwambaana namba ya simu ya Beckham na kuwa mchezaji huyo bado ni wa kutegemewa. Hata hivyo Strachan alisema ana amini Beckham hatorudi katika ligi kuu yaUingereza, matamshi yanayoashiria huenda akajiungana Celtic.

Beckham alijiunga na real Madrid kwa kitita cha pauni milion i25 kutoka Manchester United. Katika msimu huu mchezaji huyo wa kiungo amekua mara nyingi akiwekwaakiba. Kumekuweko pia na uvumi kwamba huenda Beckham akajiunga na timu moja wapo katika ligi kuu ya sokanchini Marekani.Mkataba wake na Madrid unamalizikaJanuari na iwapo hatorefusha basi atakua huru kuihama kilabu hiyo katikati ya mwaka ujao.

Ligi kuu ya England ilitimua vumbi tena Jumamosi,na Manchester United inaendelea kutamba kileleni. MANU kama inavyojulikana miamba hiyo iliibwaga Bolton Wanderers mabao 4-0, huku Wayne Rooney akiuona wavu mara tatu, na bao la nne kutingishwa na Christian Ronaldo. Sasa United ina pointi 25 baada ya mechi 10.mabingwa watetezi Chelsea baada ya kazi ngumu nayo ikaondoka na ushindi wa mabao 2-0,wakati Arsenal ilitoka sare na Everton bao 1-1. Liverpool ikaipa funzo Aston Villa la mabao 3-1 .

Kwa upande mwengine mchezaji maarufu kutoka Nigeria Nwankwo Kanu alidhihirisha kuwa bado ni wa kutegemewa aliposherehekea bao lake la saba msimu huu aliyopachika alipoipatia timu ya yake Portsmouth goli la pili katika ushindi wao wa mabao 3-1 dhidi ya Reading.

Barani Afrika CS Sfaxien ya Tunisia ilijizatiti vyema na kujiweka katika nafasi nzuri, kwa kutoka sare 1-1 na Al Ahli ya Misri mjini Cairo, katika mchezo wa kwanza wa fainali ya ubingwa wa Afrika. Pambano la marudiano la fainali hiyo ni mjini Tunis Novemba 11. Al Ahli iliokua ya kwanza kuliona lango katika mchezo wa Jumapili ndiyo mabingwa watetezi wa kombe hilo.

Kiu cha Timu ya taifa ya Nigeria ya kandanda lawanawake, kutaka kunyakua ubingwa wa tano wa kombe laAfrika, kilikumbwa na patashika, ilipoifungakwa taabu Guinea ya Ikweta mabao 4-2 licha ya kuchezanyumbani katika uwanja wa michezo mjini Warri.Mchezaji bora wa soka la wanawake barani afrikaPerpetua Nkwocha, ndiye aliyekua nyota wa pambanohilo. Katika mechi nyengine ya kundi hilo la kwanza ,Banyana Banyana ya Afrika kusini ikaibwaga Algeria mabao 4-0. Kundi B Kamerun ilitoka sare na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo 1-1 nayo Ghana ikaibwaga Mali 1-0 .

Riadha :Mkenya Wilfred Kigen jana alishinda mbio za nyika-marathon za kilomita 42 za mjini Frankfurt . Mbele ya watazamaji wapatao laki mbili, Kigen alitumia saa 2 dakika 9 na sekunde 6. Katika nafasi ya pili na ya tatu walikua ni wakenya wenzake Moses Arusei na Francio Bowen. Kwa spande wa wanawake Pavetlana Ponomarenko wa Urusi aliibuka mshindi kwa muda wa saa 2 dakika 30 sekunde 5, akifuatiwa na Kirsten Otterbu kutoka Norway.

Ama katika ringi ya mabondia, habari za kusikitisha ni kuuwawa kwa Trevor Berbick bondia wa mwisho kuchuana na mfalme wa zamani masumbwi duniani Muhammad Ali. Berbick alikutwa amekufa katika uwanja wa kanisa karibu na nyumbani kwake huko Norwich nchini Jamaica, ambalo ni eneo maarufu kwa watalii, akiwa na alama za majeraha yanayofanana na mtu aliyepigwa kwa panga.

Polisi ilisema imemtia nguvuni kijana mmoja wa kiume wa miaka 20 ambaye ni jirani yake marehemu. Berbick aliyempiga Ali katika pambano la mwisho la Mfalme huyo 1981. Alirudi Jamaica 2003 baada ya kurudishwa kutoka Marekani ambako alihusika na visa kadhaa vya uvunjaji sheria na hata kutumikia kifungo gerezani.

 • Tarehe 30.10.2006
 • Mwandishi Mohammed AbdulRahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHd2
 • Tarehe 30.10.2006
 • Mwandishi Mohammed AbdulRahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHd2