1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matokeo ya awali yampa Merkel ushindi

Mohammed Khelef
24 Septemba 2017

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani anaonekana kuelekea kushinda kwenye uchaguzi wa leo, lakini akiwa anapoteza viti vingi zaidi ya hapo kabla na huku chama cha siasa kali cha AfD kikija juu kwa kasi.

https://p.dw.com/p/2kcFu
Bundestagswahl 2017 | SPD - Martin Schulz, Kanzlerkandidat
Picha: Reuters/M. Dalder

Kansela Angela Merkel anaonekana kuumizwa kwenye uchaguzi huu kwa kupoteza asimilia kadhaa, lakini bado ndiye mwenye nafasi ya kuongoza muhula wa tatu wa ukansela.

Lakini nani atamchukuwa kuwa mshirika wake kwenye serikali ya mseto?

Tayari mgombea wa Social Democrat (SPD), Martin Schulz, ametangaza kukubali kushindwa lakini akiweka wazi kuwa hatajiunga na serikali ya mseto, na badala yake ataongoza upinzani. 

SPD imepoteza asilimia 5.3 kulinganisha na ushindi wake wa awali, huku chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, AfD, kikiongeza asilimia 8.3 kwenye bunge la shirikisho, Bundestag.

Kansela Merkel amesema kwamba alitazamia ushindi mkubwa zaidi, lakini wapigakura wameamua kuwa Ujerumani inapaswa kuongozwa kwa ushirikiano wa vyama. Na sasa kinachosubiriwa ni muungano upi utaongoza.

Zaidi angalia hapa: http://www.dw.com/sw/idhaa-ya-kiswahili/s-11588