1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matarajio mazuri kwa uchumi duniani

Maja Dreyer12 Aprili 2007

Shirika la fedha la kimataifa, IMF, katika ripoti yake mpya juu ya ukuaji wa uchumi duniani linasema uchumi ulimwenguni utakua kwa asilimia 4,9 katika mwaka ujao. Mwaka uliopita uchumi duniani ulikua kwa asilimia 5,4. Ripoti hii ni muhimu kupima hali ya uchumi na ndiyo maana hii idadi zilizotolewa ni habari nzuri kwa sekta ya biashara na kwa binadamu kwa ujumla.

https://p.dw.com/p/CHGO
Jengo la IMF mjini Washinton, Marekani
Jengo la IMF mjini Washinton, MarekaniPicha: IMF

Alipotangaza habari hizo nzuri, mkuu wa idara ya uchunguzi ya shirika la fedha la kimataifa, IMF, Bw. Simon Johnson, alionekana ameridhika kabisa hapo aliposema: “Kila mmoja ulimwenguni ananufaika kutokana na ukuaji wa uchumi. Jambo hilo no muhimu sana. Sisemi kuwa haijawahi kutokea, hata hivyo lakini ni jambo la kushangaza.”

Licha ya kuwa ukuaji wa uchumi hautarajiwi kufika kiwango cha mwaka jana, bado haijaathirika kutokana na kupunguwa ukuaji nchini Marekani na pia licha ya uhaba wa usalama kwenye soko la kifedha duniani. Bw. Johnson wa shirika la IMF alikiri kuwa Marekani inaonekana imepata mafua ya kiuchumi, lakini alivyosema Johnson haya ni mafua yasiyo mkali na ambayo hayataenea. Kwa ujumla, ukuaji wa uchumi uko katika nchi nyingi, China na India zikiendelea kugeuza mfumo wao wa biashara wakati nchi za Ulaya na Japan zinaonekana zitaishinda Marekani.

Kulingana na ripoti ya IMF, Ukuaji wa uchumi katika Amerika Kusini utapungua kwa kiasi, lakini matarajio barani Afrika ni mazuri kutokana na usalama wa kiuchumi, msamaha wa madeni kutoka wa nchi tajiri na kuongezwa vitega uchumi kutoka ngambo.

Ripoti hii ya IMF inatolewa mara mbili kwa mwaka na ni kipimo muhimu kuhusiana na uchumi duniani. Kulikuwa na hofu kwamba ukuaji wa uchumi utaweza kupungua haraka kutokana na soko la biashara kupoteza usalama wake na pia iko hatari ya uchumi wa Marekani kuanguka chini.

Huu ni mwaka wa tano uchumi wa dunia unakua vizuri, na hivyo ni muda mrefu zaidi wa ukuaji wa uchumi tangu mwanzoni mwa miaka ya 1970. Bw. Simon Johnson: “Bila shaka, baada ya kuwa na ukuaji mzuri wa uchumi, watu wanadhani kuna hatari kubwa ya mfumko wa bei. Kutokana na nchi nyingi kuongeza nafasi zao za viwanda na pia kwa sababu ya uzalishaji wa mafuta umeongezwa, naamini tutabaki na kiwango hichi cha asilimia tano katika ukuaji wa uchumi kwa muda zaidi.”

Wakati huo huo, shirika la IMF limearifu kuwa litatoa Dola Millioni 57 kwa Kenya, likisema kuwa ukuaji wa uchumi nchini Kenya umeboreka tangu mwaka 2004. Sasa inabidi mageuzi mengine yafanywe haraka pamoja na kuongeza juhudi za kujenga miundo mbinu. Katika ripoti juu ya hali ya uchumi nchini Kenya, shirika la IMF linasema hatua zilizochukuliwa na serikali ya Kenya hivi karibuni zilisaidia kuimarisha idara za serikali na kuongeza uwazi wa utawala, lakini bado linadai visa vya ulaji rushwa zinaendelea. Mwaka jana, mashirika ya IMF na Benki ya Dunia yamechelewesha kutoa mamillioni ya Dola kwa ajili ya kuisaidia Kenya kwa sababu ya ulaji rushwa.