Mataifa makuu Ulaya yapinga kuendelea mazungumzo ya Kosovo | Habari za Ulimwengu | DW | 08.12.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mataifa makuu Ulaya yapinga kuendelea mazungumzo ya Kosovo

BRUSSELS

Ujerumani,Ufaransa,Uingereza na Italia zimesema kwamba zinapinga kuendelea kwa mazungumzo juu ya mustabali wa Kosovo jimbo la Serbia .

Katika taarifa ya pamoja nchi hizo nne zimesema kundi la pande tatu la Umoja wa Ulaya,Marekani na Urusi limemaliza juhudi zote za kutafuta suluhisho.Wakosovo wa asili ya Albania walio wengi hivi sasa wanatarajiwa kujitangazia uhuru kutoka Serbia . Balozi wa Ur usi kwenye Umoja wa Mataifa Vitaly Churkis ameomba mazungumzo hayo yaendelee kati ya wahusika.

Kukiwa na uwezekano wa kuzuka kwa machafuko ya umwagaji damu Jumuiya ya Kujihami ya Mataifa magharibu NATO imeahidi kuendelea kuweka kikosi chake cha wanajeshi 17,000 huko Kosovo.

 • Tarehe 08.12.2007
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CZAk
 • Tarehe 08.12.2007
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CZAk

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com