1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa makubwa kuwasaidia waasi Syria

23 Juni 2013

Mataifa makubwa yanayounga mkono waasi nchini Syria yameamua jana Jumamosi (22.06.2013) kuwapatia waasi msaada wa haraka wa silaha ili kuweza kupambana na majeshi ya serikali na kuwalinda raia wa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/18uZ9
U.S. Secretary of State John Kerry (R) speaks during the London 11 countries "Friends of Syria" meeting in Doha June 22, 2013. Western and Arab opponents of Bashar al-Assad met in Qatar on Saturday to tighten coordination of their stepped up support for rebels battling to overthrow the Syrian president. REUTERS/Mohammed Dabbous (QATAR - Tags: POLITICS CONFLICT)
Kikao cha mawaziri wa kundi la marafiki wa Syria mjini DohaPicha: Reuters

Lakini pamoja na kwamba mataifa hayo yanajitayarisha kuongeza mchango wao katika vita hivyo ambavyo vimesababisha zaidi ya watu 100,000 hadi sasa kupoteza maisha, mataifa hayo yamedai kuwa Iran na kundi la wanamgambo kutoka Lebanon la Hizboullah kuacha kuunga mkono utawala wa rais Bashar al-Assad.

Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Qatar na mwenyeji wa mkutano huo Sheikh Hamad bin Jassem al-Thani amesema kuwa mkutano huo wa mjini Doha wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa zile nchi zinazojitambulisha kama "marafiki wa Syria", wamechukua uamuzi wa siri juu ya hatua muafaka ili kubadilisha hali ya mambo katika vita hivyo.

U.S. Secretary of State John Kerry (R) speaks during the London 11 countries "Friends of Syria" meeting in Doha June 22, 2013. Western and Arab opponents of Bashar al-Assad met in Qatar on Saturday to tighten coordination of their stepped up support for rebels battling to overthrow the Syrian president. REUTERS/Mohammed Dabbous (QATAR - Tags: POLITICS CONFLICT)
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John KerryPicha: Reuters

Taarifa ya pamoja imesema kuwa "kila nchi katika njia zake" itatoa , haraka vifaa vinavyohitajika, ili waasi waweze kupambana na mashambulizi makali kutoka majeshi ya serikali pamoja na washirika wake na kuwalinda watu wa Syria."

Baadhi wana wasi wasi

Sheikh Hamad amesema kuwa nchi mbili kati ya 11 zinazoshiriki zimeeleza wasi wasi wao, huku wanadiploamasia wakisema nchi hizo ni Ujerumani na Italia.

Wanaoshiriki wengine ni pamoja na mawaziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza, Misri, Ufaransa, Jordan , Saudi Arabia, Uturuki, Umoja wa Falme za kiarabu na Marekani.

Marekani na Qatar zimetoa wito wa kuongezwa misaada kufikisha mwisho kile ambacho waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry alichosema kuwa ni hali ya kutokuwa na uwiano katika medani ya vita.

Kerry amesema Marekani inaendelea kuhimiza mpango wa amani ambao unajumuisha kufanyika mkutano mjini Geneva pamoja na kuundwa kwa serikali ya mpito itakayochaguliwa na upande wa Assad na upinzani.

A picture shows destruction in Sbeneh, south of the Syrian capital Damascus, on June 16, 2013. More than 70 Syrian military officers have defected to the opposition and crossed into Turkey, an official there said, as world leaders prepared to discuss the Syrian conflict at the G8 summit. AFP PHOTO/WARD AL-KESWANI (Photo credit should read WARD AL-KESWANI/AFP/Getty Images)
Mapambano mjini DamascusPicha: Ward Al-Keswani/AFP/Getty Images

Hakuna uwiano

Lakini ameongeza kuwa waasi wanahitaji msaada zaidi ili kuweza kufika Geneva na kuweza kuweka hali ya uwiano katika vita.

Sheikh Hamad amerudia matamshi ya Kerry , akisema kuwa suluhisho la amani , haliwezi kufikiwa hadi pale uwiano katika vita utakapofikiwa, ili kuweza kuulazimisha utawala wa Syria kukaa pamoja na upinzani katika mazungumzo.

Siku ya Alhamis , jeshi la Syria huru limesema kuwa linahitaji silaha za kupambana na ndege za kivita pamoja na vifaru. Mwanadiplomasia wa mataifa ya magharibi mjini Doha amesema jana Jumamosi kuwa mkuu wa jeshi hilo la Syria huru , FSA jenerali Selim Idriss amewasilisha orodha ya maombi na kwamba orodha hiyo imekubaliwa kwa kiasi kikubwa.

"Kila mmoja atasaidia na kutoa msaada mzuri," mwanadiplomasia huyo amesema , na kuongeza kuwa msaada huo utakuwa muhimu na pia ni hatua muhimu ".

Mkutano huo wa Doha pia umeshutumu kuingilia kati kwa wanamgambo wa Hizboullah kutoka Lebanon pamoja na wapiganaji kutoka Iran na Iraq katika vita nchini Syria, wakidai kuwa wapiganaji hao wajiondoe mara moja katika vita hivyo.

Syria's President Bashar al-Assad gestures during an interview with journalists from Argentina in Damascus in this handout photograph distributed by Syria's national news agency SANA on May 18, 2013. SANA/Handout via Reuters (SYRIA - Tags: POLITICS CONFLICT CIVIL UNREST) ATTENTION EDITORS - THIS IMAGE WAS PROVIDED BY A THIRD PARTY. FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS. THIS PICTURE IS DISTRIBUTED EXACTLY AS RECEIVED BY REUTERS, AS A SERVICE TO CLIENTS
Rais Bashar al-AssadPicha: Reuters

Wanamgambo wa Hezboullah na wapiganaji wa Kishia kutoka Iraq pia wamekuwa wakipigana katika eneo la eneo la ibada la Washia katika mji wa Sayyid Zainab kusini mwa mji mkuu Damascus, wakati makamanda wa kijeshi kutoka Iran wanaaminika kuwa wanatoa ushauri kwa maafisa wa jeshi la Assad katika mashambulizi yao dhidi ya waasi.

Mawaziri hao wamesema kuwa kuongezeka kwa hali ya kivita ya kimadhehebu katika mzozo huo pamoja na kuingilia kati kwa wapiganaji kutoka nje, kunatishia umoja wa nchi ya Syria na kupanua mzozo huo katika eneo lote.

Pia wameeleza wasi wasi wao mkubwa kutokana na kuongezeka kwa makundi ya kigaidi pamoja na kuongezeka hali ya misimamo mikali ya kidini nchini Syria.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre / afpe / ape

Mhariri: Bruce Amani