1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashirika 12 Congo yaituhumu CENI kukiuka taratibu za zabuni

Sylvia Mwehozi
10 Septemba 2018

Mashirika 12 yanayofuatilia taratibu za uchaguzi nchini Kongo yameituhumu tume ya uchaguzi CENI kwa ukiukaji wa taratibu katika kuagiza vifaa vya uchaguzi na huduma kama vile za kisheria.

https://p.dw.com/p/34bgk
Demokratischen Republik Kongo | Wahlkommision |  Wahlautomat
Picha: DW/F. Quenum

Mashirika hayo yameilalamikia CENI hasa kuhusina na ununuzi wa computer za uchaguzi kutoka kampuni ya Meru Sytems ya Korea Kusini pasipo kupitia mchakato wa zabuni. Vipi tume huru ya uchaguzi imetumia fedha zilizotolewa na serikali katika maandalizi ya uchaguzi ?Swali hilo limesababisha ripoti ya mashirika 12 ya kiria ambayo yameelezea kwamba tume huru ya uchaguzi haiheshimu utaratibu wa matumizi ya fedha kwa ajili ya uchaguzi.

Mashirika hayo yanayotetea matumizi bora ya fedha za umma,yanaelezea kwamba CENI imekuwa ikiendesha shughuli za matumizi ya fedha kisiri siri. Hali hiyo inayapa wasiwasi kuhusiana na uendeshwaji wa taratibu za uchaguzi. 

Kufuatia nyaraka kadhaa zilizoochunguzwa na mashirika hayo ni kwamba tume ya uchaguzi imekuwa ikikiuka sheria inayotaka kutangazwa zabuni itakayofuatiwa na ukaguzi wa makampuni yanayotoa huduma kwa tume ya uchaguzi.

Demokratische Republik Kongo Wahlmaschine
Mashine za kupigia kura huko Congo Picha: Getty Images/AFP/J. Wessels

Mashirika hayo yamezungumza makubaliano yaliofikiwa kati ya tume ya uchaguzi na kampuni ya Korea ya kusini ya MERU SYSTEMS ambayo inatakiwa kuleta kompyuta laki moja kwa ajili ya shughuli za uchaguzi. Kwa mujibu wa ripoti ya mashirika hayo ni kwamba makubaliano hayo yalifanyika kisiri.

Sheria ya ununuzi inaelezea kwamba manunuzi yote ya umma yanayozidi dola laki moja ni lazima yapitie katika mchakato wa zabuni kwa kuyashirikisha makampuni kadhaa. Mashirika hayo yanaelezea pia ukiukaji wa sheria ya uchaguzi na tume hii ambayo inalazimisha kutangazwa kwa daftari ya wapigaji kura wote siku 60 baada ya operesheni ya kuandikisha wapiga kura kutangazwa. Georges Kapiamba ni kiongozi wa shirika la kiraia na la kutetea haki za binadamu, Acces a la Justice , ACAJ amesema amemuandikia mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi kuhusu ukiukaji huo wa sheria :

Juhudi za DW kupata maoni ya tume ya uchaguzi kuhusu tuhuma hizi hazikufua dafu. Mashirika hayo yameomba bunge kuendesha uchunguzi kuhusu matumizi ya bajeti ya uchaguzi na tume huru ya uchaguzi. Ikumbukwe kwamba tume hur ya uchaguzi itoa bajeti ya dola bilioni moja na kani tatu milioni kwa ajili ya maandalaizi ya chaguzi saba nchini ukiwemo uchaguzi wa rais na bunge.

Mwandishi:  Saleh Mwanamilongo,DW Kinshasa.

Mhariri: Iddi Ssessanga