Mashambulio yapamba moto Syria | Matukio ya Kisiasa | DW | 28.01.2012
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mashambulio yapamba moto Syria

Vikosi vya Syria hapo jana viliimarisha ukandamizaji wake,huku wanaharakati wakiripoti vifo 120 katika kipindi cha siku mbili na Umoja wa Mataifa ukishinikizwa kutoa mwito kwa Rais Bashar al-Assad kuondoka madarakani.

epa02893476 A grab from an undated handout video made available by Shaam News Network on its youtube channel, shows Syrian security forces clashing with protesters after the Eid al-Fitr prayers, allegedly in Nakhl area of Deraa, Syria, 30 August 2011. According to media report on 02 september 2011, At least four people were killed and dozens were injured when Syrian security forces opened fire late 01 September on pro-democracy protesters in the flashpoint city of Homs, activists based in Lebanon told the German Press Agency DPA. The United Nations says more than 2000 civilians have been killed since the protests began in mid-March 2011. Syrian President Bashar al-Assad has repeatedly blamed the unrest in his country on 'armed terrorist groups'. EPA/SHAAM NEWS NETWORK/HANDOUT BEST QUALITY AVAILABLE. EPA IS USING AN IMAGE FROM AN ALTERNATIVE SOURCE, THEREFORE EPA COULD NOT CONFIRM THE EXACT DATE AND SOURCE OF THE IMAGE. HANDOUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES

Vikosi vyaendelea kutumia mabavu

Nchini Syria, vikosi vya usalama hapo jana viliimarisha ukandamizaji wake, huku wanaharakati wakiripoti vifo vya watu 120 katika kipindi cha siku mbili na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, likishinikizwa na Ulaya na nchi za Kiarabu kutoa mwito kwa Rais Bashar al-Assad kuondoka madarakani.

Mkuu wa tume ya waangalizi wa Umoja wa Nchi za Kiarabu, Jenerali Mohammed Ahmed Mustafa al-Dabi amesema, machafuko yamepamba moto, hasa katika miji ya kati ya Homs na Hama, iliyo ngome ya upinzani pamoja na eneo la Idlib kaskazini mwa nchi. Jenerali huyo amesema, mashambulio hayo hayasaidii kuyaleta pamoja makundi yote katika meza ya majadiliano.

Siku mbili mfululizo, vikosi vya Syria viliendelea kuushambulia mji wa Homs, wakati Morocco hapo jana ikiwasilisha mswada wa azimio lililotayarishwa na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani pamoja na nchi za Kiarabu . Azimio hilo linatoa mwito kwa Umoja wa Mataifa hatimae kuchukua hatua ili kuumaliza ukandamizaji nchini Syria. Katika mswada wa azimio hilo, serikali ya Syria inatakiwa moja kwa moja kukomesha ukandamizaji, ambao Umoja wa Mataifa unasema, umesababisha zaidi ya vifo 5,400 tangu mwezi Machi.

Lakini balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, Vitaly Churkin amesema, mswada huo hauambatani na msimamo wao. Urusi inapinga cho chote kuhusiana na vikwazo, marufuku ya silaha au mabadiliko ya serikali nchini Syria. Mwezi wa Oktoba, Urusi na China zilitumia kura ya turufu kupinga azimio lililopendekezwa na Ulaya, zikituhumu kuwa nchi za magharibi zinataka mabadiliko ya serikali. Majadiliano rasmi kuhusu azimio hilo jipya, yanatazamiwa kuanza jumatatu ijayo mjini New York.

 • Tarehe 28.01.2012
 • Mwandishi Martin,Prema/afpe
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13sHQ
 • Tarehe 28.01.2012
 • Mwandishi Martin,Prema/afpe
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13sHQ

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com