1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yasema Iran inazidi kuwasaidia wanamgambo wa kujitoa mhanga Iraq

25 Julai 2007

Balozi wa Marekani nchini Iraq Ryan Crocker amesema kuwa Iran imekuwa ikiongeza msaada wake kwa makundi ya wanamgambo wa kujitoa mhanga nchini Iraq katika miezi ya hivi karibuni.

https://p.dw.com/p/CB2U
Ryan Crocker, balozi wa Marekani nchini Iraq
Ryan Crocker, balozi wa Marekani nchini IraqPicha: AP

Balozi huyo aliyasema hayo baada ya mkutano wake na maafisa wa Iran juu ya suala la usalama nchini Iraq, mkutano ambao ni watatu kati ya pande hizo mbili katika kipindi cha miongo mitatu iliyopita.

Balozi Crocker alisema Iran inachangia madhila makubwa wanayopata wananchi wa Iraq na ameitaka kueleza bayana nini inachokitaka.

Wakati huo huo watu 26 wamekufa na wengine 70 kujeruhiwa baada ya mshambuliaji wa kujitoa mhanga kujilipua katikati ya kundi la watu kwenye soko kuu la mji wa washia wa Hilla kusini mwa Iraq.

Mji huo uliyoko kiasi cha kilomita 100 kusini mwa Baghdad umekuwa ukikumbwa na mashambulio kadhaa ya kujitoa mhanga likiwemo la tarehe sita mwezi March ambapo watu 120 waliuawa.