1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yajikinga kutoka kwa makombora ya Korea Kaskazini.

19 Juni 2009

Huenda Korea Kaskazini ikalifanyia jaribio kombora la masafa marefu mwezi ujao.

https://p.dw.com/p/IUil
Waziri wa ulinzi wa Marekani Robert GatesPicha: AP

Marekani inasema kuwa imeweka makombora ya kujikinga katika kisiwa cha Hawaii baada ya madai yaliyotolewa na gazeti moja nchini Japan yaliyosema kuwa Korea kaskazini huenda ikavyatua kombora lake la masafa marefu kwenda kisiwa hicho mapema mwezi ujao.

Waziri wa ulinzi wa Marekani, Robert Gates, alisema kuwa mitambo hiyo ya kujikinga inajumuisha ile inayoweza kuhamishwa pamoja na mitambo ya rada.

Kwa upande mwingine, Marekani imeanza kuifuatilia meli ya Korea Kaskazini ambayo iliondoka katika bandari ya Korea siku ya Jumatano, baada ya nchi hiyo kuwekewa vikwazo na umoja wsa mataifa na kuruhusu kukaguliwa kwa meli zake.

Afisa mmoja kutoka Marekani anasema kuwa huenda meli hiyo imesheheni zana zlizopigwa marufuku kufuatia vikwazo vipya dbidi ya Korea kaskazi ilivyo wekewa na umoja wa mataifa.

Hii ndio meli ya kwanza kufuatiliwa tangu Korea kaskazini iwekewa vikwazo hivyo wiki iliyopita, baada ya taifa hilo la kikoministi kulifanyia jaribio kombora la kinyuklia tarehe 25 mwezi uliopita.

Bwana Gates pia alisema kuwa mitambo ya kujikinga pia imewekwa tayari katika jimbo la Alaska na kuongzea kuwa wako katika hali nzuri kulinda taifa la Marekani.

Mitambo hiyo ya kujikinga ina uwezo wa kutungua makombora ya masafa marefu. Maafisa kutoka Marekani na pia kutoka Korea kusini wanasema kuwa, huenda korea kaskazini inajiandaa kulifanyia jaribio kombora la masafa marefu baada ya majaribio kama yaliyofanyika mwaka 1998 mwaka 2006 na pia mwaka huu.

Nordkorea Kurzstreckenrakete Test
Kombora la masafa marefu lafyatuliwa nchini Korea Kaskazini.Picha: AP

Korea Kaskazini inadai kuwa ilirusha satelite angani mnamo tarehe tano mwezi Aprili lakini kwa upande mwingine Marekani na washirika wake wanaamini kuwa lilikuwa na jaribio la kombora la masafa marefu lilillo na uwezo la kufika katika jimbo la Alaska nchini Marekani.

Hali ya wasi wasi imekuwa ikiongozeka katika maeneo yanaoizunguka Korea Kaskazini baada ya kulifanyia jaribio kombora la kinyuklia mwezi uliopita.

Afisa mmoja anayehusika na ulinzi nchini Marekani alithibitisha kuwa jeshi la Marekani linaifuatilia meli ya Korea kaskazini ambayo inakisiwa kusheheni mizigo inayohusuinana na nyuklia au makombora na kwenda kinyume na vikwazo vya silaha iliyowekewa na umoja wa mataifa.

Meli hiyo huenda ikawa mtihani wa kwanza kwa umoja wa mataifa wa vikwazo vya kupiga marufu kuingizwa au kusafirishwa kutoka korea Kaskazini silaha au Teknolojia inayohusiana na silaha.

Kufuatia azimioa la umoja wa mataifa lililoungwa mkono na china pamoja na Urusi, umoja wa mataifa uliamrisha kufanyiwa ukaguzi meli, lakini haukuidhinisha kutumiwa kwa nguvu za kijeshi wakati wa ukaguzi huo.

Vikwazo hivyo vinaruhusu jeshi la wanamaji wa marekani na vikosi vingine kukagua meli za Korea Kaskazini kutoka nchi zingine zinazokisiwa kusafirisha mizigo iliyopigwa marufuku.

Siku ya Jumamosi Korea kaskazini iliapa kuwa itaunda mabomu zaidi ya atomic kama mnago mya wa silaha ikilitaja kama jibu kwa vikwazo vipya vya umoja wa mataifa.

Mwandishi :Jason Nyakundi

Mhariri :Othman Miraji