1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaiwekea vikwazo zaidi Iran

9 Julai 2008

-

https://p.dw.com/p/EYur

WASHINGTON

Marekani imeidhinisha vikwazo zaidi dhidi ya maafisa wa Iran na kampuni zinazoshukiwa kuisaidia nchi hiyo katika utengenezaji wa silaha za kinuklia.Vikwazo hivyo ni pamoja na kusimamisha akaunti na kuzuia shughuli zote za kibishara na watu sita pamoja na kampuni tano zilizotajwa na serikali na idara za fedha nchini Marekani.Tangazo hilo la Marekani limekuja wakati viongozi wa G8 wameitaka Iran kusimamisha shughuli zake za kurutubisha madini ya Uranium.Iran inakanusha madai ya nchi za Magharibi kwamba inapania kutengeneza silaha za kinuklia na kusisitiza kwamba mpango huo unadhamiriwa kwa matumizi ya amani.