1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yafungua ukurasa mpya

P.Martin9 Februari 2009

Mada iliyogonga vichwa vya habari katika takriban magazeti yote nchini Ujerumani ni kujuzulu kwa Waziri wa Fedha Michael Glos wa chama cha CSU.

https://p.dw.com/p/Gpzh

Kwa bahati mbaya magazeti yalichelewa kupata habari kuhusu mrithi wake.Atakaeshika wadhifa ulioachiliwa na Glos ni Karl-Theodor zu Guttenberg ambae hivi sasa ni katibu mkuu wa chama cha CSU.Lakini kwanza tutaanza na Mkutano wa Usalama wa Kimataifa uliomalizika siku ya Jumapili mjini Munich kusini ya Ujermani.Gazeti la HEILBRONNER STIMME linasema:

" Ujumbe uliotoka kwenye mkutano wa usalama mjini Munich ni dhahiri. Marekani imefungua ukurasa mpya. Inataka kushirikiana na washirika wake wa Ulaya na mataifa yote duniani.Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden alipohotubia mkutano huo alitoa sura ya kuvutia inayoambatana na ujumbe huo.Barack Obama alipoingia madarakani, hatua hiyo haikufungamanishwa tu na matumaini mengi kila pembe ya dunia- rais huyo mpya wa Marekani upesi iwezekanavyo anataka pia kutimiza ahadi mbali mbali alizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi.Sasa ndio imechukuliwa hatua ya mwanzo kurekebisha ushirikiano uliovurugwa wakati wa utawala wa miaka minane ya George W.Bush.

Kwa maoni ya gazeti la MÄRKISCHE ODER ZEITUNG,wenyeji wa Mkutano wa Usalama hawakutia maanani tatizo la madawa ya kulevya linaloathiri pia nchi za Ulaya-tatizo lisiloshughulikiwi kabisa na serikali ya Rais Hamid Karzai nchini Afghanistan.Likiendelea linasema:

"Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden alitangaza mkakati wa kutathiminiwa upya sera za Afghanistan.Kwani vikosi vya ziada vilivyopelekwa Afghanistan au miradi dhaifu ya kiraia haikusaidia kuleta maendeleo nchini humo tangu mwaka 2001.Badala yake hali ya usalama inazidi kuwa mbaya."

Sasa tukigeukia mada iliyogonga vichwa vya habari katika magazeti mengi ya Ujerumani leo hii - yaani kujiuzulu kwa ghafula kwa Waziri wa Fedha wa Ujerumani Michael Glos wa chama cha CSU,gazeti la BADISCHE ZEITUNG kutoka Freiburg linasema:

" Moja analoweza kudai Glos ni kuwa aliwababaisha Kansela na Mwenyekiti wa CSU.Kwani Angela Merkel na Horst Seehofer walihitaji zaidi ya saa 24 kukubali kujiuzulu kwa Michael Glos.Ionekanavyo,Glos amechoshwa na mengi.Baada ya kutotiwa maanani katika baraza la mawaziri na kuzidi kutengwa na mwenyekiti wa chama chake,Glos mwanachama wa CSU aliebobea,alitaka angalao kungatuka kwake madarakani uwe ni uamuzi wake,lamalizia BADISCHE ZEITUNG.