1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yafikiria uwezekano wa kuzidisha wanajeshi Irak-New-Yorks Times

16 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCin

New-York:

Kwa mujibu wa ripoti ya New York Times,rais George W. Bush wa Marekani anapanga kutuma wanajeshi 20 elfu zaidi nchini Irak.Gazeti la New York Times likimnukuu afisa wa ngazi ya juu serikalini,limesema viongozi wa kijeshi wanachunguza maombi ya ikulu ya Marekani na kutathmini namna ya kuzidishwa na kugharimiwa wanajeshi hao ziada.Kamisheni ya baraza la Congress iliyoongozwa na waziri wa zamani wa mambo ya nchi za nje James Baker ilishauri wanajeshi wa Marekani wahamishwe hadi ifikapo mwaka 2008 na juhudi za kideplomasia ziendelezwe ,zikijumuishwa pia Syria na Iran.