1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na Urusi kuanza mazungumzo ya kuimarisha uhusiano kati yao.

Jason Nyakundi6 Mei 2009

Suala la kupunguzwa kwa silaha za nuklia kwenye ajenda..

https://p.dw.com/p/HkrN
Waziri wa masuala ya kigeni wa marekani Hillary Rodham Clinton.Picha: AP

Miezi miwili iliyopita suala la kuboresha uhusiano kati ya Marekani na Urusi liling´oa nanga lakini hata hivyo uhusiano huo umeingiliwa kati na suala la kupunguzwa kwa silaha pamoja na mzozo nchini Georgia.

Waziri wa masuala ya kigeni wa marekani Hillay Clinton anatarajiwa kukutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov mjini washington siku ya Alhamisi ukiwa ni mkutano wao wa pili tangu mazungumzo yao ya kwanza mjini Geneva mwezi machi mwaka huu na kuanza kwa uhusiano mpya kati ya Marekani na Urusi.

Afisa mmoja kutoka Marekani anasema kuwa tangu kufanyika kwa mkutano huo wa Geneva ishara kutoka nchini urusi hazieleweki na haifahamiki ikiwa Urusi ingetaka kupita hatua gani kuimarisha uhusiano kati yake na Marekani.

Mzozo mpya wiki hii kati ya Urusi na Georgia ambapo Georgia inaishutumu Urusi kusaidia jaribio lililoshindwa la mapinduzi ya kijeshi huenda yakagubika mazungumzo kati ya clinton na Lavrov.

Sasa changamoto kubwa ni jinsi ya kuboresha uhusiano huo na kutimiza ahadi ya suala la kupunguzwa kwa silaha

Urusi ilipigana vita na jirani wake Georgia mwaka uliopita suala ambalo lilisababisha kuharibika kwa uhusiano kati ya Urusi na Marekani pamoja na washirika wake.

Sergei Lavrov Hillary Clinton
Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov pamoja na waziri wa masuala ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton.Picha: AP

Suala lingine ni mvutano kati ya Urusi na jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi NATO baada ya kutimuliwa kwa wanadiplomasia wawili wa Urusi waliyokuwa na makao ya NATO mjini Brussels nchini Ubelgiji ambao ni wafanyakazi wa jumuiya hilo wiki iliyopita.

Afisa mmoja kutoka marekani alisema kuwa uamuzi wa Lavrov wa kubadili mipango yake ya kuhudhuria mkutano kati ya Urusi na NATO mwezi huu ulikuwa mzuri kwa kuwa ni jambo ambalo lingemgadhabisha Clinton ambaye aliitisha mkutano huo wa Washington baada ya ule wa kwanza kutupiliwa mbali kufuatia vita kati ya Urusi na Georgia.

Wataalamu wanasema kuwa nafasi nzuri ya kuwepo kwa mafanikio ya mapema ni kwenye majadiliano yatakayochukua mahala pa mkataba wa vita baridi wa kupunguza silaha.

Mazumgumzo hayo yanatarajiwa kufikia mwisho mwezi Disemba mwaka huu na pande husika zinasema kuwa matokeo yanastahili kuwa yamepatikana.

Mazungumzo ya kwanza muhimu yanatarariwa kuandaliwa mjini Moscow mei 18 kabla ya rais wa Marekani Barack Obama kukutana na rais wa Urusi Dmitry Medvedev mwezi Julai mwaka huu.

Marekani inataka kupunguzwa kwa silaha za kinyulikia suala ambalo pia urusi inalifahamu. Charles Kupcham mtaalamu kutoka urusi anasema kuwa Marekani hatua hizi za marekani zinatatikana kuonyesha matokeo muhimu.

Kupcham hata hivyo alisema kuwa kuna vizingiti kadha hasa katika upande wa Urusi likiwemo suala la mgogoro wa kiuchumi duniani.

Mwandishi: Jason Nyakundi/RTR

Mhariri: Othman Miraji