1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na china

29 Julai 2009

Ushirikiano mpya wa kiuchumi:

https://p.dw.com/p/IzSf
Timothy GeithnerPicha: AP

Katika kikao cha cha siku mbili cha kutunga mkakati wa pamoja na ushirikiano wa kiuchumi mjini Washington ,Marekani na Jamhuri ya Watu wa China, zimetunga ajenda mbali mbali juu ya ushirikiano wao.kikao hicho kilichoandaliwa pamoja na waziri wa nje na wa fedha wa Marekamni na kushiriki wajumbe 150 kutoka China, mbele kabisa ulikuwa msukosuko wa uchumi ulimwenguni,nishati na sera za kutunza hali ya hewa lakini pia maeneo ya mzozo ya wakati huu ulimwenguni.

Mkutano huu ulilenga hasa kujuana pande hizo mbili na kumsikiliza mwenzake ana msimamo gani juu ya maswali fulani.

Maafikiano yamepatikana kati ya dola kuu ya kiviwanda-Marekani na China yenye akiba kubwa ya fedha hasa juu haja ya kushirikiana mno kabisa katika sekta ya sera za uchumi na fedha.Pande zote mbili zinatambua kwamba hatua ya kila mmoja inazochukua zinaathiri na kushawishi uchumi wa dunia .Kwahivyo, pande hizo mbili zina azma ya kuendeleza sera zao za kuchumi hata ingawa chini ya masharti mengine.Marekani inataka mno kuyaongoza kisheria masoko yake ya fedha wakati china inataka kuimarisha ununuzi wa bidhaa nchini.Mahusiano ya kibiashara kati ya China na Marekani yanakusudiwa kuimarishwa zaidi na biashara ya dunia kukuzwa .China inakusudia kufungua zaidi masoko yake na kuruhusu raslimali za kigeni katika taasisi zake za mikopo.

Kuhusu swali hili waziri wa fedha wa Marekani Timothy Geithner alisema:

"Tumeafikiana mpango wa kujenga msingi wa kukuza uchumi kwa njia za usawa kati ya nchi zetu mbili na wa dunia."

Nae mshauri wa utawala uliopita wa george Bush kwa maswali ya kusini-mashariki mwa asia, Dennis Wilder asema,

"Kutoka uchumi unaelekeza kuuza bidhaa nje na kuelekea ule wa kuhimiza mahitaji ya bidhaa nchini na hivyo kuwa na usuhuba wa aina nyengine wa kibiashara na Marekani ,kwa upande wa china si jambo la leo na kesho."

Baada ya mazungumzo yao juu ya sera za kutunza mazingira na hali ya hewa, dola hizo mbili zilitia saini tangazo la nia yao kufanya hivyo.Tangazo hilo kimsingi limetaja kwamba katika sekta ya mabadiliko ya hali ya hewa,kutunza mazingira na kujipatioa nishati inayopatikana tena na tena-renewable energy",Marekani na china zinapanga kushirikiana kwa nguvu zaidi.Hazikutoa lakini shabaha maalumu za kufikia.Kwa maoni ya Dennis Wilder , juu ya hivyo hayo ni mafanikio.Kwani huo anaona ni mwanzo kuona msimamo wa serikali mpya ya marekani unafahamika zaidi katika swali la mabadiliko ya hali ya hewa.

Machina huwa wanajizuwia linapikuja swali la kuweka shabaha maalumu kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa kwa gesi zinazopaa hewani.Wanaona kunazuwia ukuaji wake wa uchumi. Hayo amesema Dennis Wilder,aliekua mshauri wa rais aliepita george Bush na bingwa wa maswsali ya kusini mashariki mwa asia katika Baraza la usalama wa taifa.

Anasema:

" Wakati wa mazungumzo, machina wamearifu kwamba, ni taitizo lao la kipindi kirefu kufanya hivyo na kwamba, haitakua rahisi kurekebisha mfumo wa uchumi wao .Hatahivyo, machina wengi wanatambua kwamba wakati umewadia kuanza hivyo."

Mwandishi:Bergmann,Christina

Mhariri:M.Abdul-Rahman