1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani kupunguza idadi ya wanajeshi kutoka Irak

Josephat Charo22 Desemba 2007

Idadi ya wanajeshi wa Marekani nchini Irak itapunguzwa kutokana na kuimarika kwa usalama na kupungua kwa machafuko

https://p.dw.com/p/CfEu
Waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates

Waziri wa ulinzi wa Marekani, Robert Gates, amesema Marekani itaondoa vikosi vyake vitano vya wanajeshi karibu 20,000 kutoka nchini Irak ifikapo katikati ya mwaka ujao 2008.

Akizungumza kwenye mkutano wa mwaka na waandishi wa habari, waziri Robert Gates amesema hilo litawezeka kwa sababu ya ufanisi uliofikiwa na wanajeshi katika kudumisha usalama.

Bwana Gates ameongeza kusema, ´Tumaini langu limekuwa hali halisi nchini Irak itaendelea kuw anzuri kiasi kwamba wakati jenerali Petreaus na makamanda wa jeshi watakapofany atathmi ni yao mwezi Machi mwakani, tutaweza kuendelea kupunguza idadi ya wanajeshi´.

Wizara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon, imesema machafuko nchini Irak yamepungua kufuatia hatua ya kuongeza idadi ya wanajeshi kufikia 160,000.