1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAPUTO : 60,000 wahamishwa kutokana na mafuriko

12 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSz

Wanajeshi na wafanyakazi wa uokozi wakitumia helikopta na mitumbwi wamewahamisha takriban watu 60,000 kutoka Bonde lililofurika la Mto Zambezi katikati ya Msumbiji ambapo maisha ya watu wengine zaidi ya 100,000 yako hatarini.

Mvua zaidi zimetabiriwa kunyesha na milango ya kudhibiti mafuriko ambayo lazima ifunguliwe ili kuokowa ukuta wa bwawa kubwa kabisa la kuzalisha umeme kwa nguvu za maji kutazidi kuzidisha hatari kwa maisha ya watu hao.

Watu 100 wamezama au kupoteza maisha yao kwa kurushwa na umeme kutokana na waya za umeme zilizozama majini na mamia kwa maelfu wamelazimishwa kuacha makaazi yao kutokana na mvua hizo kubwa zilizokumba eneo kubwa la kusini mwa Afrika kuanzia Angola upande wa magharibi hadi Msumbiji upande wa mashariki na Malawi,Zambia na Zimbabwe kwa upande wa kati kati.

Maelfu ya hekta za mazao zimeharibiwa na madaraja na barabara kuanguka na kusombwa na maji.