1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

maporomoko ya matope yaua zaidi ya 50 Java

26 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/CgPn

JAVA

Zaidi ya watu 50 inahofiwa wamefariki na wengine wengi hawajulikani waliko katika kisiwa cha Java nchini Indonesia kufuatia maporomoko ya matope yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha kwa muda wa saa 12.

Maporomoko hayo ya matope yametokea leo hii katika maeneo ya Karanganyar na Wonogiri .Shughuli za uokoaji zimetatizwa na hali mbaya ya mtelezo na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.Mvua hiyo imesababisha mafuriko katika katika visiwa vya Java ,Sumatra pamoja na Sulawesi.