1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano yazuka upya Mashariki mwa Kongo

4 Septemba 2008

Nchini Kongo mapigano yanaripotiwa kuzuka upya baina ya waasi wanaoongozwa na Jenerali muasi Laurent Nkunda na wanajeshi wa serikali ya Kongo kwenye eneo Tamugenga mkoani Kivu ya Kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/FBUf
Mapigano dhidi ya waasi wa Laurent Nkunda Mashariki mwa Kongo yazuka upyaPicha: AP

Mapigano hayo yalitokea kufuatia maandamano ya raia wa Rutchuru hapo jana ambapo kifaru kimoja cha jeshi kilichomwa na wanajeshi wawili wa Umoja wa Mataifa kujeruhiwa.Itakumbukwa kuwa makubaliano ya amani yalitiwa saini mwezi Januari mwaka huu japo mapigano bado yanazuka mara kwa mara.

Kutoka Goma mwandishi wetu John Kanyunyu ametuandalia taarifa ifuatayo.