1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano yanaripotiwa katika mitaa kadhaa ya Tripoli

25 Februari 2011

Utawala wa Libya unazidi kulaaniwa kwa kutumia maguvu ya kijeshi dhidi ya waanmadamani.Waandamanaji watano wameuwawa leo hii katika mtaa moja wa mji mkuu Tripoli.

https://p.dw.com/p/10PbR
Maandamano ya Benghazi,mashariki ya LibyaPicha: AP

Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi anazidi kubanwa kwa upande mmoja na upande wa upinzani unaodai kulikomboa eneo la mashariki huku mapigano makali yakiendelea katika eneo la magharibi na kwa upande wa pili jumuia ya kimataifa inayozidi kumtia kishindo asitishe umwagaji damu.

Mnamo siku ya 11 ya uasi dhidi ya utawala wa kanali Muammar Ghaddafi anayewatuhumu wapinzani wake kuchochewa na mtandao wa kigaidi wa Al Qaida unatapa tapa huku, juhudi za kimataifa zimeshika kasi.

Katika wakati ambapo malalamiko yanayoonyesha kuenea kutoka Benghazi hadi magharibi ya mji mkuu Tripoli, miji ya mwambao au ile iliyoko karibu na mwambao, ambayo sehemu yake kubwa ni jangwa imesalimika na mapigano.

Rückkehr eines Tunesiers aus Libyen
Wageni wanaipa akisogo LibyaPicha: DW

Katika wakati ambapo eneo la Mashariki, tajiri kwa mafuta linaonyesha kudhibitiwa na wapinzani, wanaharakati wanaopinga utawala wa Ghaddafi wanajiandaa kuelekea Tripoli kwa lengo wanasema la kumng'oa madarakani kanali Ghaddafi. Katika maeneo ya mji huo mkuu vikosi vya polisi vinapiga doria karibu na misikiti yote ya mji mkuu huo. Habari zinasema vikosi vya usalama vimewafyetulia risasi waandamanaji katika mtaa wa-Djanzour. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, watu wasiopungua watano wameuwawa.

Mapigano yameripotiwa pia katika mitaa ya Ben Achour, Tajoura na Ghout Achaal mjini Tripoli.

Wakihutubia baada ya sala ya Ijumaa maimamu wametoa mwito wa kurejea hali ya utulivu na kukoma vitendo vya uharibifu. Kwa mujibu wa waumini, maimamu hao wamelazimishwa na serikali kusema hivyo.

Deutschland Libyen Deutsche kehren aus Tripolis zurück
Wajerumani hao wameyapa kisogo machafuko nchini LibyaPicha: picture alliance/dpa

Nje ya Libya laana zinazidi kutolewa dhidi ya utawala wa Libya unaonyesha kuachwa mkono na washirika wake wa nchi za kiarabu na mabalozi wake kadhaa ikiwa ni pamoja na yule wa mjini Paris na katika shirika la Umoja wa mataifa la elimu sayansi na utamaduni, UNESCO.

Rais Abdullaye Wade wa Senegal amelaani vikali matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji nchini Libya.

Baraza la haki za binaadamu la Umoja wa mataifa linakutana kuzungumzia hali nchini Libya.

Licha ya yote hayo Seif Al Islam mmojawapo wa watoto wa kiume wa kanali Gaddafi amesema katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Uturuki, kwamba familia yake itasalia kwa kila hali nchini Libya na ameonya "hawatoachia sehemu ya nchi yao kudhibitiwa na magaidi.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Afp,Reuters

Mhariri: Josephat Charo