1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano yaingia mitaa ya Gaza.

Eric Kalume Ponda15 Januari 2009

Mapigano yangali yakiendelea huko Gaza baada ya Wanajeshi wa Israel kuingia katika mitaa ya mji wa Gaza na kufanya mashambulio makali usiku kucha,hali iliyosababisha maelfu ya raia wa mitaa hiyo kutoroka makaazi yao.

https://p.dw.com/p/GYpj
Moshi ukitanda katika baadhi ya mitaa iliyoshambuliwa wanajeshi wa Israel mjini GazaPicha: AP


Mapigano yangali yakiendelea huko Gaza baada ya Wanajeshi wa Israel kuingia katika mitaa ya mji wa Gaza na kufanya mashambulio makali usiku kucha,hali iliyosababisha maelfu ya raia wa mitaa hiyo kutoroka makaazi yao.


Mashambgulizi hayo yameendelea huku kukukiwa na matumaini ya pande mbili kwenye mzozo huo kukubali mapendekezo yaliyomo kwenye mpango wa amani unaoongozwa na Misri. Jamii ya kimataifa imeimarisha juhudi zake za kutafuta amani katika eneo hilo la Ukanda wa Gaza huku katibu mkuu wa Umoja wa mataifa akitarajiwa kufanya mashauriano na viongozi wa Israel juu ya kusimamishwa mapigano hayo..


Ni oparesheni kali iliyoendeshwa na wanajeshi wa Israel katika mitaa ya mji wa Gaza ambako wanajeshi hao walishambulia jumla ya vituo 70 vinavyodaiwa ghala ya zana za kijeshi za wafuasi wa chama cha Hamas.


Wakati wa mashambulio hayo wapiganaji wawili wa Hamas waliuawa wakati wa mashambulizi hayo katika maeneo yenye idadi kubwa ya watu mjini Gaza.


Mashambulizi hayo yalisambaa hadi mji wa kusini wa Khan Yunis na Jabiliya katika eneo la Kaskazini. Wakaazi waliojawa na ho walilazimika kukimbnilia usalama wao katika Hospitali zilizopo karibu kutoroka mapigano hayo ambayo yanaingia siku yake ya 20.


Kwa kujibu mashambulizi hayo wafuasi wa chama cha Hamas pia walivurumisha makombora 14 ya Maroketi nadni ya Issrael ingawa hakuna habari zozote zilizotolewa kuhusu majeruhi.


Mashambulizi ya leo yametokea siku moja tu baada ya wajumbe wa chama cha Hama wanaohudhuria mashaurinao ya mpango wa amani unaoongozwa na Misri mjin i Cairo kuridhia mapendekezo yaliyomo kwenye mpango huo, hali iliyotoa mwangaza kwamba huenda amani ikaafikiwa katika eneo hilo la mashariki ya kati.


Kiongozi wa chama cha Hamas kwenye ujumbe huo Ismail Haniya alisema baada ya kukamilisha mashauriano hapo jana kuwa Hamas wako tayari kukomesha mashambulizi yao iwapo mapendekezo yao waliyowasilisha kwenye mpango huo wa amani yatakubaliwa. Masharti hayo ni pamoja na Israel kukomesha mashambulizi na kuondoka katika ardhi ya Gaza bila ya masharti na kufunguliwa kwa maeneo yote ya mpakani.


Upande wa Israel bado unasubiriwa kuwasilisha mapendekezo yake wakati mjumbe maalum Amos Gilad akitarajiwa kuwasili mjini Cairo kwa mashauriano hayo.



Wakati huo huo katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon amefanya mashauriano na viongozi wa Israel huku akisisitisha kukomeshwa kwa vita hivyo. Akiwa katika siku ya pili ya ziara katika juhudi za kutafuta kusitishwa kwa vita hivyo Ban Ki- Moon aliikumbusha Israekl na mataifa yote ulimwenguni kwamba yanawajibuka kwa baraza la usalama la Umoja wa mataifa. Hali kadhalika katibu mkuu huyo anatarajiwa kuwa na mazungumzo na kiongozi wa Wa-Palestina Mahamud Abbas ba pia kuzuru Gaza.


Habari zaidi zasema kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank Walterv Steinmeier amewasili nchini Israel katika ziara yake kutoa msukumo zaidi ya kukomeshwa kwa mashambulizi katika eneo la ukanda wa Gaza.


Hii ni ziara ya pili ya waziri huyo katika eneo hilo ambapo wakati wa ziara yake ya kwanza akishirikiana na Rais Hosni Mubarak wa Misri walitangaza mapendekezo ya mpango wa amani.


Bw Steinmeier anatarajiwa kuwa na mazungumzo na waziri wa wa mambo ya nchi za nje wa Israel Tzipi Livni na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-Moon.


Hadi kufikia sasa jumla ya Wapalestina 1,041 wameuawa na wengine 4,85o kujeruhiwa huku Israel ikipoteza wanajeshi 10 na raia watatu. tangu vita hivyo vilipoanza tarehe 27 mwezi uliopita.


Ponda -Afp