1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano yachacha Cote d'Ivoire

Thelma Mwadzaya3 Aprili 2011

Mapigano kati ya wafuasi wa mahasimu wawili wa kisiasa nchini Cote d’Ivoire yameingia siku yake ya tatu katika mji mkuu wa Abidjan.

https://p.dw.com/p/10mgZ
Laurent Gbagbo anayeng'ang'ania madarakaPicha: picture alliance / dpa

Vikosi vinavyomtii Alassane Ouattara anayetambuliwa na jamii ya kimataifa kama rais halali wa nchi hiyo, vinaripotiwa kupambana na wanajeshi wanaomuunga mkono Laurent Gbagbo.

Kiongozi wa zamani wa wapiganaji vijana wa Alassane Ouattara,Damana Picas amewatolea wito wapambe wao kupambana na mahasimu wao.

Elfenbeinküste Wahl und Unruhen Flash-Galerie
Mji mkuu wa Abidjan umegubikwa na mapiganoPicha: picture alliance/dpa

Laurent Gbagbo anaendelea kung'ang'ania madaraka na wanajeshi wake wanaripotiwa kuwa wanakidhibiti kituo cha televisheni cha taifa. Laurent Gbagbo amewatolea wito wafuasi wake kuelekea barabarani na kupambana.Wakati huohuo,Marekani imemtaka Laurent Gbagbo kuachia madaraka haraka iwezekanavyo kwani anauhatarisha usalama katika nchi hiyo ya Afrika magharibi.