1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano mapya yatokea Cote d'Ivoire

Thelma Mwadzaya24 Februari 2011

Kiasi ya watu 15 wameuawa katika mapigano mapya yaliyotokea Cote d'Ivoire pale wanajeshi wanaomuunga mkono Laurent Gbagbo walipolivamia eneo ambalo ni ngome ya mpinzani wake mkuu Alassane Ouatarra.

https://p.dw.com/p/10OjE
Laurent Gbagbo wa Cote d'IvoirePicha: picture alliance / dpa

 Siku moja kabla, wafuasi hao wa Ouatarra walifanikiwa kuwafurusha wanajeshi wa hasimu wake. Ghasia hizo zinatokea wakati ambapo juhudi za kuutanzua mzozo huo kidiplomasia zinaendelea. Mapema wiki hii jopo maalum la marais liliizuru Abidjan na wakakutana na washirika wakuu wa kisiasa wa Cote d'Ivoire. Mzozo huo wa kisiasa umesababishwa na mvutano kati ya Alassane Ouatarra na mpinzani wake mkuu Laurent Gbagbo wanaodai kuwa washindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi Novemba mwaka uliopita.

Elfenbeinküste Thabo Mbeki Besuch
Alassane Ouatarra akiwa na rais wa zamani wa Afrika Kusini,Thabo MbekiPicha: AP