1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mapigano kati ya Israel na Hamas

Waziri wa nje wa Israel ameitaka jumuia ya kimataifa iwashinikize Hamas waache mashambulio. Serakali ya Israel imeitaka jumuia ya kimataifa iwashinikize wapiganaji wa Hamas kukomesha mashambulizi ya maroketi dhidi ya Israel, la sivyo Israel haitovumilia mashambulizi hayo ya Hamas.

Mashambulio jijini Gaza City

Mashambulio jijini Gaza City

Hayo yamesemwa leo na waziri wa mambo ya nchi za njee wa Israel Tzipi Livni,

Akiwahutubia mabalozi karibu 100 walioko nchini Israel ,waziri wa mambo ya nchi za nje wa Israel Tzipi Livni alisema, mashambulizi ya maroketi ya kundi la Hamas, kusini mwa Israel ni kitendo ambacho hakivumiliki na jumuia ya kimataifa imekua ikilichukulia jambo hilo kua nila kawaida .

Waziri Livni amesema Israel, sasa imechoshwa na mashambulizi hayo.

Karibu makombora 50 ya kundi la Hamas yameweza kuvurumishwa nchini Israel, siku chache zilizopita ,na kuwajeruhi raia sita wa Israel, na bado Hamas inaendelea na hujuma za makombora yake dhidi ya Israel.

Ijuma nne iliopita ndege za kivita za Israel zilianza mashambulizi katika mji wa ghaza ,haya yakiwa ndio mashambulizi ya kwanza, kwa muda wa miezi sita iliopita.

Mpaka sasa inasemekana wapiganaji 13 wa kundi la Hamas pamoja na vijana wawili wakipalastina wameuwa katika mashambulizi hayo ya Israel.

Mashambulizi haya ya Israel ndani ya ghaza, huenda yakaufanya mzozo huu kupanuka zaidi,

kundi la Fatah na kundi la Hamas kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuvunjilia mbali serakali ya kitaifa.

Nae Mfalme wa Jordan, Abdullah wa pili, amewataka wapalastina waondowe tafauti zao, na ameonya kua , mashambulizi ya Israel, yatazidi kuifanya hali ya raia wapalastina kua mbaya.

Wakati huo huo mwangaaza umeanza kuchomoza katika mkutano wa bishara wakimataifa , unaofanyika mjini Amman Jordan .

Wajumbe wa palastina na wajumbe wa Israel wamekubaliana katika mkutano huo kuunda baraza la pamoja la kibiashara, ili kukuza uchumi katika nchi zao, na pia kuendeleza mikakati ya kutafuta Amani, baina ya wapalastina na wa Israel.

Baraza hilo litakua na watu kumi kutoka nchi zote mbili, wote wakiwa wafanya biashara maarufu .

 • Tarehe 18.05.2007
 • Mwandishi Omar Mutassa
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHE7
 • Tarehe 18.05.2007
 • Mwandishi Omar Mutassa
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHE7

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com