1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri.

Sekione Kitojo30 Aprili 2007

Rheinische Post kutoka Düsseldorf linaeleza kuwa viwanda vinavyotumia chuma vimepata mapato makubwa kutokana na soko la dunia la chuma kuwa zuri: Kitojo: Lakini hali hii linaandika gazeti hilo haipaswi kuwa hivyo daima dumu. Mada kuu zilizowashughulisha wahariri leo hii ni kuhusu tahadhari ya kufanyika mgomo wa wafanyakazi wa makampuni ya viwanda vya chuma na Electroniki katika wakati baada ya sherehe za Mei mosi, na pia hali ya vyama vya wafanyakazi kwa jumla. Pia wahariri wanaizungumzia hali ya mambo inavyoendelea nchini Uturuki.

https://p.dw.com/p/CHT5

Katika mada ya kwanza gazeti la Na hali yake inayofahamika sana ya kutafuta uwezekano wa kupunguza gharama za uzalishaji inakuja na athari kadha za hapo baadaye, kwa viwanda hivi , hususan kwa watu wa kati kutokana na kupunguza matumizi. Kwa hiyo kutakuwa na majadiliano juu ya kupandisha mishahara kwa asilimia nne au zaidi, hali ambayo inaweza kuleta hapo baadaye uwezekano wa migomo, ambapo vyama na wanachama wake mara fulani waliweza kufanikisha, lakini kutokana na duru hii ya mabadiliko ya gharama wanaweza kuichochea hali hiyo.

Katika duru za kiuchumi inafahamika wazi, kuwa inaonekana hakuna makubaliano ya maana yatakayopatikana kama linavyoeleza gazeti la Nordkurier kutoka Neubrandenburg.

Tatizo ni kwamba : mzozo huu wa viwango gani vitolewe, unajielekeza katika masharti yanayotolewa na vyama vikubwa vya wafanyakazi. Ukichukua kwa mfano chama cha IG Metall kinadai asilimia 6,5, na wakati huo huo viwanda vidogo vidogo vinakufa. Madai halisi yanayoweza kukubalika , sio tu yanaweza kuwafurahisha wafanyabiashara , bali pia vyama vya wafanyakazi vyenyewe linasema gazeti la Nordkurier.

Gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung linaangalia majadiliano katika viwanda vya kemikali na ujenzi na kutoa mifano kuwa .

Katika pande zote hizo mbili kuna uhusiano wa ushirikiano wa kupandisha kiwango cha mshahara kwa nusu kutoka asilimia nne iliyopo hivi sasa. Pande zote hizo mbili zilikubaliana kulipwa kwa mkupuo kwa mujibu wa makubaliano yatakayofikiwa. Kwa hiyo vyama vya wafanyakazi vingeweza kutabiri matokeo ya matakwa yao.

Na kutoka nje ya nchi magazeti ya Ujerumani yamejishughulisha na hali ya mambo katika nchi ya Uturuki. Magazeti yanaadika kuwa Uturuki hivi sasa imejiweka katika mtihani mkubwa kuhusiana na mwelekeo wa Demokrasia nchini humo kama linavyoandika gazeti la Der Tagesspiegel la mjini Berlin.

Kutokana na mzozo juu ya uchaguzi wa rais hali haiko shwari kati ya wale wanapenda kutenganishwa kati ya dola na dini na wale wenye msimamo mkali wa dini ya Kiislamu, pamoja na wale wanaompinga kiongozi wa chama cha AKP- Erdogan kama inavyoonekana. Linakuja swali lakini hapa , iwapo utawala uliochaguliwa kidemokrasia unaweza kutimiza sera zake za kisiasa, bila ya taasisi ambayo si ya kidemokrasi kuingilia kati. Jibu la swali hili halitaathiri tu hali ya Uturuki binafsi, lakini pia nafasi yake ya kujiunga na umoja wa Ulaya.

Hali inaelekea tena kuwa kama ilivyokuwa katika mwaka 1980, ambapo kulifanyika mapinduzi nchini Uturuki ? Linauliza gazeti la Frankfurter Rundschau.

Gazeti hili linadai kuwa , halihisi hivyo. Linasema gazeti hilo kuwa Majenerali wa jeshi la Uturuki wameweza kwa kipindi kirefu kubadilisha utaratibu wao wa kuingilia kati masuala ya kisiasa. Sio kama kitu cha siri , bali ni hali iliyotolewa wazi kwa dunia nzima kufahamu, ikiwa ni mbinyo maalum unaoelekezwa mahali maalum.

Tayari hali imeonekana kutokana na kuondolewa kwa waziri mkuu mwenye msimamo mkali wa dini ya Kiislamu Erbakan mwaka 1997. Mapinduzi hayapaswi tena kufanyika , unatosha mbinyo wa tahadhari wa kutokea mapinduzi, linadokeza gazeti la Frankfurter Rundschau.

Naam hadi hapo ndio tunakamilisha udondozi wa maoni ya wahariri wa magazeti ya leo hapa Ujerumani.