1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini.

Abdu Said Mtullya9 Julai 2009

Katika maoni yao leo wahariri wa magazeti ya Ujerumani wanazungumzia juu ya mkutano wa nchi tajiri G8, mjini L'Aquilla.

https://p.dw.com/p/IkIG
Viongozi kutoka nchi tajiri, G8 kwenye mkutano wao mjini L'Aquilla.Picha: AP


Wahariri wa magazeti ya Ujerumani karibu yote leo wanatoa maoni yao juu ya mkutano wa nchi tajiri , G8 unaoendelea mjini L'Aquilla.

Mhariri wa gazeti la Westfällische Nachrichten anaezungumzia suala la mabadiliko ya hali ya hewa linalozingatiwa na viongozi wa G8 kwenye mkutano wao mjini L'Aquilla, nchini Italia anasema kuwa anaetaka kutunza mazingira hana budi alizingatie kwa makini suala la mabadiliko ya hali ya hewa. Mhariri huyo anasisitiza kuwa janga la kuzidi kuongezeka kwa joto duniani linahitaji hatua za haraka.

Gazeti la Badische pia linazungumzia suala la mabadiliko ya hali ya hewa kwa kusisitiza kwamba hakuna kinachoweza kufikiwa ikiwa nchi zinazoinukia kiuchumi hazitashirikishwa katika msingi wa usawa.Gazeti hilo linasema la muhimu kuuliza ni hatua gani zitachukuliwa na nchi zinazoinukia kiuchumi kama India na China.? Ni jambo la uhakika nchi hizo hazitatoa kauli za kujiwajibisha juu ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Nchi hizo mbili na nyingine zote zinazoendelea zinatumai kupata manufaa fulani kwenye mkutano juu ya hali ya hewa utakaofanyika mjini Copenhagen mnamo mwezi wa Desemba. Gazeti la Badische linaeleza kuwa, kwa mtazamo wa nchi zinazoendelea, nchi tajiri zinapaswa kubeba mzigo mkubwa katika kukabiliana na tishio la mabadiliko ya hali ya hewa.

Gazeti la Rhein Necker linasema katika siku ya kwanza jana, mengi yalifikiwa kwenye mkutano wa G8 mjini L'Aquilla hata hivyo, mhariri wa gazeti hilo anaeleleza kuwa hakuna kilichofikiwa kwa uhakika.

Mhariri huyo anasema ni kweli kwamba Marekani ,China na India kwa mara ya kwanza zimetambua mwambatano uliopo kati ya hewa chafu na kuongezeka kwa joto duniani. Hayo tayari ni mengi, anasema mhariri huyo, lakini ambacho hakijafikiwa ni uamuzi wa kisheria wa kuonesha ni nchi gani, na kwa kiasi gani zinapaswa kupunguza utoaji wa gesi zinazoongeza joto duniani.


Mwanidshi/Mtullya A.

Mhariri/Miraji Othman