1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini.

Mtullya, Abdu Said8 Julai 2008

Magazeti karibu yote , katika maoni yao leo yanazungumzia juu ya mkutano wa viongozi wa nchi tajiri G8 nchini Japan.

https://p.dw.com/p/EYWM
Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini na Waziri mkuu wa Japan Yasuo Fukuda kwenye mkutano wa G8.Picha: AP

Wahariri wa magazeti karibu yote,leo wanazungmzia juu ya mkutano wa viongozi wa nchi tajiri unaoendelea nchini Japan. Na mhariri wa gazeti la Badische Zeitung anachambua sababu zinazowafanya matalibani wawe maaruf nchini Afghanistan.

Juu ya mkutano wa viongozi wa nchi tajiri unaohudhuriwa pia na viongozi kutoka nchi za Afrika gazeti la Münchner Merkur linasema orodha ya matatizo yanayopaswa kutatuliwa ni ndefu sana kiasi kwamba huenda , mwishowe viongozi kwenye mkutano huo wa nchini Japan wakaondoka mikono mitupu. Gazeti la Münchner Merkur linasema uzoefu umeonesha kuwa viongozi hao hukubaliana juu ya mambo mengi lakini bila ya kuwajibika kuyatekeleza.

Gazeti la Lausitzer Rundschau pia linatoa maoni juu ya mkutano huo nchini Japan kwa kusema kwamba watu wanafikiri ,njaa barani Afrika inasababishwa Berlin,Brussels au New York.

Mhariri wa gazeti hilo anaeleza kwamba baadhi ya madai yanayotolewa dhidi ya nchi tajiri G 8, yanasikika kana kwamba njaa iliyopo barani Afrika inatokana na matukio ya nje tu. Mgogoro wa njaa barani Afrika hautaweza kutatuliwa kwa mtazamo kama huo. Gazeti linakumbusha juu ya vita katika sehemu kadhaa katika bara hilo, pamoja na migogoro ya kisiasa kama vile nchini Zimbabwe.Gazeti hilo linasema rushwa pia inasababisha njaa katika nchi za Afrika.Gazeti la Nordwest-Zeitung linasisitiza juu ya ulazima wa nishati ya nyuklia katika kukabiliana na mfumuko wa bei ya nishati duniani. Lakini pia linasisitiza umuhimu wa kusonga mbele na utafiti wa kutafuta nishati endelevu.

Mhariria wa gazeti hilo anasema katika maoni yake, kuwa ni muhimu kutafuta nishati mbadala, lakini hakuna anaeweza kukwepa kabisa, matumizi nishati ya nyuklia.

Gazeti la Badische Zeitung linatoa maoni juu ya shambulio la kujitoa mhanga kwenye ubalozi wa India nchini Afghanistan.

Gazeti hilo linasema lengo la mataliban ni kuitia dosari serikali ya Afghanistan.

Na hakika inafanikiwa, siyo kwa sababu tu, ya udhaifu wa majeshi ya usalama za nchi hiyo. Gazeti linasema rushwa inayotendeka ndani ya serikali inachangia sana katika kuitia dosari serikali hiyo.