1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani.

7 Januari 2008

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wanazungumzia kuhusu uwezekano wa kuzipa makali zaidi adhabu kwa vijana wanaotenda uhalifu.

https://p.dw.com/p/ClMB

Mjadala kuhusu uwezekano wa kuzipa makali zaidi adhabu kwa vijana wanaotenda uhalifu, unachukua nafasi ya juu kabisa katika maoni ya wahariri katika magazeti ya Ujerumani hii leo. Mada hii pia inahusika na kuikagua serikali ya muungano pamoja na chama cha SPD. Aliyewakusanyia maoni hayo ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo ni Sekione Kitojo.

Gazeti la Süddeutsche Zeitung kutoka Munich linakosoa msimamo wa kansela Merkel, wa kukimbilia kuzipa makali zaidi adhabu hizo kwa vijana kinyume na alivyoahidi. Gazeti linaandika:

Kwa hiyo kansela ameshindwa kuvumilia, kwa kile ambacho amekifanyia kazi kwa nguvu kabisa. Kila mara alikuwa anazungumzia na kusisitiza msimamo wa kati katika masuala ya siasa za jamii. Anaufanya hauna maana mkutano wake juu ya kuzijumuisha jamii kama vile anavyofanya waziri wa mambo ya ndani Wolfgang Schäuble na mkutano wake na Waislamu, anakiuka msimamo wa kauli mbiu ya mkutano mkuu wa mwisho wa chama chake , wa kukiweka chama chake katika mrengo wa kati, hali hii inaonyesha udhaifu wa mbinu. Na anajihatarishia kukiuka mipaka kwa kuunga mkono kampeni inayotoa hamasa ya kuwabana watu kutoka mataifa ya nje na kufanikisha mapambano mengine ya uchaguzi kwa CDU. Kwa hiyo kampeni hii inatenganisha pale ambapo wengine wangependa kuweka umoja.

Gazeti la Wiesbadener Kurier linashambulia moja kwa moja.

Kwamba mwenyekiti wa chama Angela Merkel pamoja na msaidizi wake Roland Koch kinyume na tamko lao la mwanzo wanaweza kwenda umbali wa kuunga mkono hili, hii inaonesha ni vipi uchaguzi katika jimbo la Hessen ulivyomgumu kwa mtazamo wa chama chao. Christian Wulff kutoka katika jimbo la Niedersachsen, hatima yake itajulikana hapo Januari 27, wadhifa wake wa uenyekiti umo katika hatari. Pamoja na hayo kwa upande wa chama cha CDU , uchaguzi huo sio jambo la dharura. Lakini kwa upande wa Koch binafsi , ambaye katika miezi michache hapo nyuma alionekana kuwa mshindi dhahiri, hivi sasa anawasiwasi. Ndio sababu , anapambana, ndio sababu kinapambana pia chama chake kwa mara nyingine tena kwa kutumia mada hii ya raia wa kigeni hapa nchini.

Na ndio sababu ya kutaka kupambana katika kinyang’anyiro hiki cha uchaguzi. Lakini mtu anapaswa kuzungumza kwa mtazamo ambao hautamwingiza katika hatia. Lakini inawezekana mtu akazungumzia suala hili.

Gazeti la Frankfurter Rundschau linajaribu kukosoa, lakini linaelekeza lawama zake kwa chama cha SPD.

Siku ya kwanza ya mwaka mpya imeonyesha wazi mkanganyiko katika chama cha SPD. Hisia zinaonyesha kuwa chama hicho hakina mkakati imara. Chama hicho kinakosa mada muhimu, kinaangalia masuala yanayojitokeza kwa taratibu mno, kama hali inavyojitokeza ya uhalifu wa vijana , na kama hapo kabla , chama hicho hakina jibu, kuhusiana na mahitaji ya kuweka utulivu na sheria kufuatwa ambayo wahafidhina wanajaribu kuisukuma. Kwa hiyo chama cha SPD kinajipeleka katika nafasi ngumu pamoja na mwenyekiti wao katika mwaka ambao utakuwa na maamuzi mengi. Chama cha Social Democratic ni lazima katika mwaka 2008 kijitambue, iwapo kinataka kuwa chama chenye nguvu katika serikali ama Kurt Beck mwenyekiti wa chama hicho atakuwa akikosoa tu kila kitu kibaya ambacho kitafanywa na kansela Merkel.

Gazeti la Münchener Merkur katika mada ya sheria ya adhabu kwa vijana linaona si vizuri kuizungumzia serikali ya muungano ama chama cha SPD.

Hali hii ni kama kuruka majivu na kukanyaga moto. Vijana walimpiga mtu mmoja vibaya sana baada ya kutoka katika treni na baada ya hapo wanasiasa wanaharibu zaidi. Kuimarisha adhabu kwa vijana kwa serikali ya muungano kunampatia mwenyekiti wa chama cha SPD Beck , kura ya turufu imara kabisa. Huu ni mwanzo wa kutatua matatizo ya uchaguzi. Ni sawa kabisa watu kuchukua hatua, kwa kuwa ni mahitaji ya usalama wao. Wanachangia kama walipa kodi , fedha nyingi kwa ajili ya mahakama , polisi na vyama na wanapaswa kusikia mipango imara , na kujua ni kwa nini washambuliaji hawa waliweza kujiamini na kufanya uhalifu huo.

Hayo msikilizaji ndio maoni ya wahariri wa magazeti ya leo hapa Ujerumani.