Maoni ya wahariri wa magazeti na Abdu Mtullya | Magazetini | DW | 30.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Maoni ya wahariri wa magazeti na Abdu Mtullya

Katika maoni yao wahariri wa magazeti ya hapa nchini leo wanazungumzia tena juu ya kitendo cha aibu kilichofanywa na askari wa Ujerumani nchini Afghanistan na juu ya mkasa uliotokea kwenye pwani ya Lebanon kati ya manowari ya Ujerumani na ndege za Israel.

Ndege za kivita za Israel ziliruka usawa wa manowari ya Ujerumani na inasemekana kuwa makombora yalifyatuliwa! Kwa bahati njema hapakua na madhara.Lakini tukio hilo limesababisha ngozi za kimbimbi ,mijini Jerusalem na Berlin

Juu ya hayo mhariri wa gazeti la NORDWEST ZEITUNG la mjini Oldenburg anatilia maanani kuwa jukumu la linalotekelezwa na jeshi la majini la Ujerumani katika pwani za Lebanon linaandamana na hatari nyingi.

Lakini mhariri huyo anataka habari zaidi zitolewe kwa wananchi. Watu wanataka kujua ni kwa kiasi gani majeshi ya Ujerumani ni salama katika pwani za Lebanon?

Mhariri wa gazeti la BERLINER ZEITUNG anasema ni muhimu uwazi ufahamike juu ya utekelezaji wa azimio la baraza la Usalama namba 1701kuhusu kusimamisha mapambano nchini Lebanon.Mhariri analalamika kuwa uwazi huo haupo. Kinachofahamika ni kwamba jeshi la maji la Ujerumani limepelekwa katika mashariki ya kati ili kuilinda Israel. Hayo ni sawa kabisa anasema mhariri, lakini huo ni upande mmoja tu wa ukweli. Gazeti la BERLINER ZEITUNG linasisitiza katika maoni yake ; kwa kuwa majeshi ya Ujerumani yapo mashariki ya kati, ni wajibu wa seriakli ya Ujerumani kueleza wazi kuwa majeshi hayo pia yatawajibika juu ya usalama wa Lebanon.

Naye mhariri wa gazeti la NÜRBERGER ZEITUNG katika maoni yake anaandika kana , kwamba, anauliza jee hatukuyasema hayo, kwamba pana hatari ya majeshi ya Ujerumani kupamnbana ana kwa ana na majeshi ya Israel katika mashariki ya kati?.

Na hayo ndiyo hasa yaliyotokea anasema mhariri huyo. Hivyo basi gazeti hilo linaitaka serikali ya Ujerumani izirudishe nyumbani manowari zote.

Mhariri wa gazeti la WIESBADEN KURIER anamtaka waziri wa ulinzi wa Ujerumani bwana Franz -Joseph Jung atumie kauli za uwazi katika mazungumzo yake mjini Jerusalem na Beirut.

Kadhalika mhariri wa gazeti anaitaka Israel itamke wazi iwapo majeshi ya Ujerumani yamepokelewa kama wasaidizi katika kulinda amani ama kama maadui.

katika maoni yao wahariri wa magazeti ya hapa nchini leo kwa mara nyingine wanazunguzmia juu ya kitendo cha aibu kilichofanywa na wanajeshi wa Ujerumani nchini Afghanistan.

Wanajeshi hao wamepigwa picha wakifurahia fuvu la binadamu kana kwamba ni nyara.

Juu ya hayo mhariri wa gazeti la FRANKFRURTER RUNDSCHAU anasema , pana haja ya kuzungumzia kwa makini zaidi juu ya jukumu la jeshi la Ujerumani katika kulinda amani nchini Afghnaistan .Lazima ifahamike wazi ni kwa muda gani jeshi hilo litatekekelza jukumu hilo kablya ya kusahaulikamiongo i mwa wananchi .