1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri na Abdu Mtullya

11 Oktoba 2006

Rais Vladmir Putin wa Urusi anaendelea na ziara ya nchini Ujerumani amekutana na mwenyeji wake Kansela Angela Merkel katika mji wa Dresden. Katika maoni yao wahariri wa magezeti ya hapa nchini leo wanazungumzia juu ya ziara hiyo

https://p.dw.com/p/CHUj

Rais Vladmir Putin wa Urusi anaendelea na ziara ya nchini Ujerumani amekutana na mwenyeji wake Kansela Angela Merkel katika mji wa Dresden.

Katika maoni yao wahariri wa magezeti ya hapa nchini leo wanazungumzia juu ya ziara hiyo

Gazeti la OSTSEE-ZEITUNG la mjini Rostock linasema:

rais Putin na Kansela Merkel wamekutana katika masafa ya usawa. Lakini masuala ya kuuawa kwa mwandishi habari Anna Politkovskaya na haki za binadamu yamezingatiwa ngwazoni.

Uhusiano wa kiuchumi baina ya Urusi na Ujerumani unaendelea kwa mwendo wa kasi .

Urusi sasa siyo tu kuwa ni mwuuzaji mafuta na gesi, bali pia wajasiramali wa nchi hiyo wanaingia katika soko la Ujerumani.Mhariri anatahadhirisha kuwa hayo yanaweza kusababisha matatizo.

Naye mhariri wa gazeti la RHEIN-NECKER ZEITUNG anatilia maanani katika maoni yake kwamba Urusi inatafuta rafiki katika Ulaya ya magharibi, rafiki atakaeiamini Urusi huku amefumba macho. Rafiki atakaeinadi demokrasia ya bwana Putin kama alivyofanya kansela wa hapo awali bwana Gerhard Schröder . Katika hayo Urusi ipo tayari kutoa vivutio , ikiwa pamoja na kuhakikisha ugavi wa nishati.

Ujerumani inahitaji uhakika huo. Kansela Merkel anatambua hayo vizuri sana lakini pamoja na hayo Kansela huyo angalau ameweza kumfanya rais Putin atoe japo machozi bandia juu ya kuuawa kwa mwandishi habari Anna Politkovskaya.

Gazeti la LANDESZEITUNG la mji wa Lüneburg linasema katika maoni yake wakati wa kukumbatiana sasa umeshapita.

Kansela Angela Merkel alikuwa mwananchi wa Ujerumani Mashariki na hivyo basi aliweza kuona jinsi himaya ya kisoviet ilivyosambaratika. Hayo yanamfanya awe katika hali ya kuweza kuitathmini Urusi vizuri zaidi, tofauti na bwana Schröder alietaka kuitambua demokrasia ya mkakasi ya rais Putin.

Rais Putin amehakikisha kwamba uchunguzi utafanywa juu ya kuuawa kwa mwandishi huyo. Hakikisho hilo limetokana na msimamo wa Kansela Merkel.

Mhariri wa gazeti KÖLNER STADT-ANZEIGER anatilia maanani kwamba Urusi inazidi kuwa muhimu kwa Ujerumani kama mgavi wa nishati na kama nchi hiyo ingelikuwa huru, hakuna angelikuwa na kipingamizi chochote, lakini uhusiano baina ya Urusi na Ujerumani haupo hivyo.Yapo maswali ya kuuliza.

Gazeti la BERLINER MORGENPOST linazungumzia juu ya kuongezeka nauli katika usafiri wa reli.

Mhariri wa gazeti hilo anasema ,kama kampuni ya reli ingelikuwa ya mtu binafsi , ongezeko hilo la nauli kunzia mwaka ujao lingekubalika. Lakini hilo ni shirika la umma ambalo kwa kiwango kikubwa linadhibiti bei. Hatahivyo ni sawa kwa meneja wa shirika hilo kujaribu kusawazisha mahesabu yake kwa kupandisha nauli.Lakini, anasema mhariri wa gazeti hilo,njia hiyo haitasaidia kwa kutambua kwamba nauli za ndege ni nafuu sana hapa nchini.