1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri juu ya Syria

Abdu Said Mtullya28 Agosti 2013

Wahariri hao leo wanazungumzia juu ya mgogoro wa Syria, haki za wanawake nchini Ujerumani na juu ya mkasa wa aliekuwa Rais wa Ujerumani Christian Wulff.

https://p.dw.com/p/19XsD
Makumu wa Rais wa Marekani Joe Biden
Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden .Picha: Reuters

Juu ya mgogoro wa Syria gazeti la "Nürnberger Nachrichten" linanatoa tahadhari kwa nchi za magharibi Mhariri wa gazeti hilo anasema Syria siyo sawa na Iraq. Lakini pilika pilika zinazoenekana sasa zinamfanya mtu aingiwe wasi wasi kwamba kosa la miaka ya nyuma litarudiwa tena.

Mhariri wa "Nürberger Nachrichten" anesema mpaka sasa hakuna ushahidi wa kuthibitisha, ni nani aliyeitumia gesi ya sumu. Wataalamu wa Umoja wa Mataifa walipaswa kukusanya ushahidi na kuufanyia tathmini. Lakini inavyoelekea Marekani haina subira.

Ushahidi wa Marekani utatiliwa mashaka:

Gazeti la "Badische" pia linatoa maoni juu ya mgogoro wa Syria.

Mhariri wa gazeti hilo pia anakumbusha juu ya yaliyotokea mnamo miaka ya nyuma. Anasema mengi yatategemea na iwapo Marekani itaweza kuthibitisha madai kwamba majeshi ya Assad yalitumia gesi ya sumu.Ikiwa ni kweli kwamba Assad alizitumia silaha za kemikali,dunia haitapaswa kukubali. Lakini mpaka sasa hakuna ushahidi wowote.Hata hivyo ushahidi wowote utakaotolewa na Marekani utatiliwa mashaka ,kwani dunia bado haijasahau kilichoitwa ushahidi uliowasilishwa na nchi hiyo kuthibitisha kwamba Saddam Hussein alikuwanazo silaha za maangamizi.

Christian Wulff mahakamani:

Gazeti la Sächsische" linatoa maoni juu ya mkasa wa aliyekuwa Rais wa Ujerumani, Christian Wulff, ambaye sasa anakabiliwa na mashtaka ya rushwa. Mhariri wa gazeti hilo anasema Bwana Wulff hakustahili kuwa Rais wa Ujerumani na kwa hivyo ilikuwa sahihi kwake kujiuzulu mwaka uliopita. Na mhariri wa gazeti la "Neue Osnabrücker" anasema Christian Wulff sawa na binadamu wengine amefanya makosa, na labda tabia yake ilienda kombo.Lakini mambo siyo mabaya kwa kiasi kinachozungumziwa. Hata hivyo kadhia zilizomhusu yeye na walio karibu naye, zinatosha kuwa mfano kwa wote.

Wanawake bado wanapunjwa:

Gazeti la "Mittelbayerische" linazungumzia juu ya haki za wanawake nchini Ujerumani. Gazeti hilo linasema kuwapo kwa takwimu zinazothibitisha kupunjwa kwa wanawake katika jamii ya Ujerumani ni kashfa kubwa.Lakini swali ni vipi jamii ya Ujerumani itaweza kuleta haki katika uwiano baina ya majukumu ya kazini na ya nyumbani kwa akina mama? Suala la usawa linawahusu wote, wanawake na wanaume nchini Ujerumani.

Mwandishi: Mtullya Abdu.Deutsche Zeitungen.

Mhariri: Josephat Charo