Maoni ya wahariri juu ya matokeo ya mkutano wa Annapolis | Magazetini | DW | 29.11.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Maoni ya wahariri juu ya matokeo ya mkutano wa Annapolis

Leo hii ikiwa ni siku moja baada ya mkutano wa Annapolis huko Marekani kumalizika, wahariri wanachunguza matokeo yake, ambayo hasa ni makubaliano kati ya Wapalestina na Waisraeli kuweka ratiba kwa mazungumzo ya amani.

default

Kushikana mikono kuna maana gani?

La kwanza ni gazeti la "Mitteldeutsche Zeitung" ambalo limeandika hivi:

“Tukiangalia ratiba hiyo ya mazungumzo inaonekana kama Rais Bush wa Marekani amejiwekea lengo kubwa la kufikia suluhisho la kuwepo dola mbili, Israel na Palestina, kabla ya muhula wake madarakani kumaliza. Huenda mara nyingine ratiba ni chombo kizuri cha kulazimisha uamuzi, lakini watu wa Mashariki ya Kati hawapendi kutoa uamuzi wakishinikizwa kufanya hivyo. Mengi yanategemea ikiwa pande zote mbili zitaweza kuhifadhi sifa yao. Na hiyo itachukua muda, tena muda mrefu.”

Ukiendelea na mhariri wa “Märkische Oderzeitung” naye anatoa onya kutokuwa na matumaini makubwa juu ya matokeo ya mkutano Annapolis. Ameandika:


“Yule anayesema matokeo haya ni mafanikio, basi hafahamu hali halisi. Kwa upande mmoja ni kweli kwamba mazungumzo ya amani ambayo yalikwama tangu muda mrefu yameanzishwa tena. Lakini upande mwingine mambo yalibadilika huko Mashariki ya Kati. Siku hizi, Wapalestina wanapigana wenyewe kwa wenyewe. Kundi lenye msimamo mkali wa Kiislamu Hamas linadhibiti eneo la ukanda wa Gaza, na huko ukingo wa Magharibi mwa mto Jordan anayetawala ni rais Abbas. Hata hivyo, Hamas hakualikwa Annapolis.”


Zaidi juu ya suala hilo tunasoma katika gazeti la “Stadtanzeiger” la mjini Cologne. Mhariri huyu anaangalia hasa washirika wawili muhimu kwenye mkutano wa Annapolis, waziri mkuu Ehud Olmert wa Israel, na rais Mahmud Abbas wa Wapalestina:


“Mabwana hao Olmert na Abbas wanataka amani. Katika rasimu ya pamoja iliyozungumziwa hadi saa za usiku wanasisitiza shahaba yao hiyo. Juu ya hayo walikubaliana juu ya ratibu ambayo yawezi kutekelezwa. Kwa hivyo walizusha matarajio mengi. Kuyatimiza lakini itakuwa kama mwujiza.”


Na hatimaye huu hapa uchambuzi wa gazeti la “Berliner Morgenpost”:


“Mkutano wa Annapolis ni mwanzo wa mgawanyiko kati ya wale wenye msimamo mkali nchi Iran kwa upande mmoja na nchi na makundi ya nchi za Kiarabu zenye siasa za wastani na ambazo zinataka amani. Lengo la juhudi hizo na rais Bush ni kuzituliza nchi kama Sudan, Syria, Pakistan au Indonesia, yaani nchi za Kiislamu zenye Wasuni wengi kupitia mazungumzo kati ya Israel na Wapalestina. Wakati huo huo, Bush anaongeza shinikizo dhidi ya Iran iliyo nchi ya madhehebu ya Kishia.”

 • Tarehe 29.11.2007
 • Mwandishi Maja Dreyer
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CUWv
 • Tarehe 29.11.2007
 • Mwandishi Maja Dreyer
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CUWv