1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Trump adanganya kuhusu vikwazo kwa wakimbizi

7 Machi 2017

Rais Donald Trump hatokubali kukiri kwamba amefanya kosa katika jaribio lake la kwanza. Mwandishi wa DW Miodrac Zoric anasema katika maoni yake amedanganya kidogo katika jaribio lake la pili.

https://p.dw.com/p/2Yl1p
USA Trump Rede vor dem Kongress
Picha: Reuters/J. Lo Scalzo

Ni waziri wake na sio rais aliyetangaza vikwazo vipya kwa wakimbizi kuingia Marekani. Waandishi hawakuruhusiwa kumuuliza waziri masuali yoyote yale.

Wananchi wa Marekani walipata picha moja tu wakati Trump alipokuwa akisaini amri yake hiyo juu ya mada ambayo ni kipenzi chake kikubwa kama alivyokuwa akiiruudia mara kwa mara wakati wa kampeni ya uchaguzi mwaka jana. Mada ambayo ndio iliomfanya achaguliwe na Wamarekani wengi kulinda mipaka ya Marekani kwa kuruhusu wakimbizi wachache tu kuingia nchini humo.

Trump mpya ambaye sio wa kawaida akikwepa kamera na vipaza sauti ambao ndio ulikuwa msingi wake ndio sababu mwishoni mwa juma aligonga vichwa vya habari kwa tuhuma nzito dhidi ya mtangulizi wake. Akidai kwamba Barack Obama aliamuru kutegesha mawasiliano ya simu katika kituo chake cha kampeni ya uchaguzi .Madai hayo yasiokuwa na uthibitisho linaendelea kubakia kuwa kosa kwa Trump.  

Vyombo vya habari ambavyo anavichukia mno inaliona hilo kuwa ni jaribio la wazi kuhamisha nadhari kutoka matatizo mengine yanaoukabili utawala wake.Urais wake umekuwa ukikabiliwa na kashfa baada ya kashfa tokea kuanza kwake.

Soric Miodrag Kommentarbild App
Mwandishi wa DW Soric Miodrag.

Wingi wa viti bungeni

Licha ya chama chake kuwa na wingi wa viti bungeni ameshindwa kupitisha hata sheria moja.Inawezekana kwamba washauri wake wamemshauri apunguze kwa kiasi fulani kuandika katika mtandao wa Twitter na kujitokeza kwenye televisheni jambo ambalo kwa vyo vyote vile haliwezi kudumu kwa muda mrefu. Mara ya mwisho rais huyo alisababisha vurugu katika viwanja vya ndege. Mahakama za Marekani zitashughulikia watu waliokamatwa kinyume na sheria kwa maoni yoyote yale utawala huu utaendelea kushikilia sera yake ya kuweka vikwazo kwa wanoingia nchini humo.

Serikali ya Marekani imeipa mgongo dunia nzima. Nchi hiyo ndio sababu ya kuwepo kwa mzozo wa wakimbizi kwa hatua zake za kuingilia kati.Trump sasa anajificha nyuma ya kuta za Ikulu. Jambo hili lina kitu fulani cha ishara.

Uongozi ni jambo tofauti aidha Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ambaye atakuwepo Washington kwa wiki moja atalizungumzia suala la mzozo wa wakimbizi ni suali.Na iwapo itakuwa hivyo itabidi iwe kwa tahadhari.Merkel anashuku kwamba Dolad Trump hatobadili kabisa sera yake ya  kujitenga.Marekani ni kwanza ni imani yake. Kansela inabidi aheshimu hilo halikadhalika nchi nyengine za Umoja wa Ulaya lakini umoja huo unaweza ukajifunza kutokana na hilo. Iwapo Marekani ina shauku ya kuwakilisha maslahi yake Waulaya wanapaswa kuwa sahihi.

Mwandishi. Miodrag Zoric/Mohamed Dahman

Mhariri: Yusuf Saumu